KWELI TENA! NAKUPONGEZA WEWE KAMISHNA JENERALI WA MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA JAMES WILBERT KAJI...HONGERA | ZamotoHabari.


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

HONGERA Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya James Jaki.

Hongera kwasababu unastahili kupewa hongera kwa kazi kubwa ambayo unaifanya ndani ya mamlaka hiyo katika kukomesha biashara ya dawa za kulevya nchini.

Ndio hongera kwababu utendaji wako na usimamizi wako kwenye kuisimamia mamlaka hiyo kumeleta matokeo makubwa sana ya kiutendaji.Mamlaka hiyo chini ya uongozi wako imeendelea kuwa imara katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Chini ya uongozi wa Kaji kwa kushirikiana na wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali kwenye mamlaka hiyo leo tunashuhudia kazi kubwa na nzuri ya kukomesha biashara hiyo.Hongereni Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.Mnastahili kusifiwa.

Kwa kazi nzuri inayofanywa na Kamishna Jenerali Kaji pamoja na mamlaka anayoingoza , imemfanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli kuamua kumteua Kaji kuwa Kamishna Jeneralali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.Kabla ya uteuzi huo Kaji alikuwa Kaimu Kamishna Jenerali katika mamlaka hiyo.

Rais Magufuli akiwa Ikulu ya Chamwino Mjini Dodoma wakati anazungumza na viongozi wa ngazi mbalimbali kwenye Serikali ya Awamu ya Tano ambapo kulikuwa na sherehe za uapisho wakurugenzi alitumia nafasi hiyo kuelezea utendaji kazi wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.Rais alielezea jinsi mamlaka hiyo inavyofanya kazi zake na kubwa zaidi kinachofanyika kinaonekana huku akijata matukio kadhaa ya ukamataji wa dawa za kulevya.Limo tukio la ukamataji bangi wilayani Meru.

Rais Magufuli wakati anatoa pongezi hizo kwa Mamlaka hiyo ndipo akatangaza na kumteua Kaji kuwa Kamishna Jenerali.Kwa Kaji haikuwa akitarajia kama Rais angemteua  kwenye nafasi hiyo.Hongera Kamisha Kaji kwa uteuzi huo.Rais Magufuli anaimani kubwa na wewe (Kamishna Jenerali).

Watanzania tunaimani kubwa na wewe.Uwezo ambao umeonesha hapo awali unatoa picha halisi ya uwezo wako mkubwa wa kuisimamia mamlaka na hatimaye nchi yetu sasa tumefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa biashara ya dawa za kulevya.

Nakumbuka na Watanzania wanakumbuka wakati Serikali ya Awamu ya Tano inaingia madarakani, Rais Magufuli alikwenda kuzindua shughuli za Bunge la 11 na katika hotuba yake alitoa maelekezo kwa Mamlaka hiyo ya nini inatakiwa kufanya kukomesha biashara ya dawa za kulevya.Hakika maelekezo ya Rais kwa Mamlaka hiyo yamekuwawa dira muhimu ya mafanikio.

Tanzania yetu leo iko salama zaidi ,biashara ya dawa za kulevya imepungua sana.Ndio biashara hiyo imepungua kwasababu Mamlaka iliamua kusimama imara.Imetumia mbinu zake za kila aina kuwabana waliokuwa wanajihusisha na mtandao wa biashara hiyo.Hakika kuna mafanikio makubwa ambayo Mamlaka hiyo imeyapata katika kipindi cha miaka mitano ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Kwanini tunampongeza Kamishna Jenerali James Kaji? Ni kwasababu anastahili pongezi hizo kutokana na mafanikio lukuki yaliyopatikana.Miongoni mwa mafanikio hayo ni maboresho ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya ambayo yalifanyika mwaka 2017, Utoaji wa Elimu kuhusu madhara ya Dawa za Kulevya, Mamlaka kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu imeweza kuanzisha vilabu vya kupinga dawa za kulevya mashuleni.

Pia kutoa elimu bora kuhusu tatizo la dawa za kulevya kwa umma wa Watanzania  kupitia vyombo mbalimbali vya habari kama vile Televisheni, magazeti, warsha za kitaifa na makongamano pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu madhara ya dawa hizo pamoja na udhibiti wa uchepushwaji wa kemikali bashirifu. Hiyo imesaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia wimbi la vijana kuingia kwenye matumizi na biashara ya dawa hizo.

Mafanikio mengine ni Kubaini na Kuvunja Mitandao mikubwa ya Dawa za Kulevya Nchini ambapo Mamlaka kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali za Kimataifa kama vile UNODC, Interpol, DEA, CIA na NCA imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhoofisha na kuvunja mitandao mikubwa ya wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ndani na nje ya Nchi.

Kwa kukumbusha tu taarifa ya mwaka 2019 ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), nchi yetu ilifanikiwa kupunguza uingizaji wa dawa za kulevya kwa asilimia 90. Pia, Mamlaka imeshinda Kesi kubwa za wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya.

Ngoja nikueleze vizuri mafanikio mengine ni kukamata wafanyabiashara wa Dawa za Kulevya ambapo kwa kipindi cha miaka mitano toka mwaka 2015 hadi  Juni, 2020, jumla ya kilo 188,489.93 za bangi kilo 124,080.33 za mirungi kilo 58.46 za Cocaine, na kilo 635.57 za heroin, zimekamatwa.

Katika ukamataji huo, jumla ya watuhumiwa 73,920 walikamatwa. Mamlaka imefanikiwa kufanya ukaguzi katika Makampuni 167 yanayojihusisha na uinngizaji wa kemikali bashirifu. Katika ukaguzi huo, Mamlaka imefanikiwa kukamata kiasi cha lita za ujazo 480,000 na kilo 22,145 za kemikali bashirifu zilizoingia nchini bila ya kufuata utaratibu.

Pamoja na hayo Mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka mitano ya Serikali ya Awamu ya Tano imefanya  upanuzi wa Huduma za Tiba kwa Waathirika wa Dawa za Kulevya. Mamlaka kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Taasisi zingine zisizo za Kiserikali imefanikiwa kupanua huduma za tiba kwa waathirika wa dawa za kulevya nchini, ambapo hadi mwaka 2016 kulikuwa na Vituo vitatu tu nchini ambavyo vilihudumia Waathirika 3,500.

Pia kumekuwa na ongezeko la vituo vitano zaidi na hivyo kufanya jumla yake kuwa vituo nane hadi Machi 2020 vikihudumia waathirika 8,500 kila siku. Mamlaka imekuwa ikisimamia upatikanaji wa uhakika wa dawa ya methadone kwa ajili ya tiba ya waraibu wa Heroin kwa kusimamia uagizaji, usambazaji na udhibiti wake.

Mamlaka imefanikiwa kuimarisha ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya na uhalifu wa kupangwa kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Taifa linaloshughulikia Masuala ya Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) pamoja na Taasisi nyingine za Kimataifa.

Tatizo la Dawa za Kulevya linavuka mipaka ya nchi yetu, hivyo ushirikiano umeelekezwa zaidi katika kubadilishana taarifa za kiintelijensia na operesheni za pamoja. Hata hivyo mwaka 2019 nchi yetu iilisaini Mkataba na Msumbiji na Afrika ya Kusini kuhusu  udhibiti wa usafirishaji wa dawa za Kulevya katika njia ya kusini kwa kuwa wafanya biashara wengi wakubwa wamehamia katika nchi hizo baada ya udhibiti kuwa mkali nchini.

Kwa maelezo hayo kiduchu tu ndio maana naona kuna kila sabababu ya Mamlaka hiyo inayoongozwa Kamishna Jenerali Kaji kupogezwa.Ndio lazima tuwapongeze kwa kazi nzuri  wanayoifanya kwa niaba ya Watanzania wengine.Huku mtaani mateja wamepungua sana.

Wauza unga wako kwenye wakati mgumu.Hawana pakutokea, wamebanwa kila kona.Kweli tena.Kaji ameamua,mamlaka imeamua kukomesha biashara ya dawa za kulevya.Tunatakiwa kuwaunga mkono kadri ya uwezo wetu.Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana.Hakuna kitakachoshindikana chini ya uongozi wa Kamishna Jenerali James Kaji na wasaidizi wake wote.

Itoshe kueleza tu ni matumaini yangu na huenda ndio matumaini ya wengi kwamba Kamishna Jenerali ataendelea na kasi yake aidha kuiongeza zaidi katika kupambana na biashara ya dawa za kulevya.Anafanya kazi nzuri ndani ya mamlaka hiyo,ni wajibu wetu kumuombea kwa Mungu ili atekeleza vema majukumu yake.

Kabla ya kuhitimmisha nisisitize jambo moja,nalo ni kwamba Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inatekeleza shughuli zake kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Mwaka  mwaka 2017/18 – 2019/20. Mpango Mkakati huo unaainisha Dira, Dhima na malengo makuu manne (4) yanayoiongoza Mamlaka katika utekelezaji wa majukumu.

Malengo hayo ni Kudhibiti Upatikanaji wa Dawa za Kulevya (Supply reduction), Kupunguza Uhitaji wa Dawa za Kulevya (Demand reduction), Kupunguza Madhara ya Matumizi ya Dawa za Kulevya (Harm reduction) na Kuimarisha Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya (International cooperation).

Nimemaliza na unachotakiwa kubaki nacho kichwani ni kitambua dhamira yangu ilikuwa kumpongeza Kamishna Jenerali James Kaji kwa kuteuliwa na Rais kwenye nafasi hiyo.

Kwa umuhimu mkubwa nakupongeza Kamishna Jenerali James Kaji.Hayo mengine niliyoeleza yakikuchosha achana nayo ingawa ndio ukweli.Tunampongeza kwasababu amefanya mambo makubwa katika kuisimamia na kuiongoza mamlaka hiyo.

Ahsante kwa kusoma nilichoandika na hasa pongezi zangu kwa Kamishna Jenerali Kaji.

Simu 0713833822
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya James Jaki.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini