Maandalizi ya eneo la jukwa kuu ambalo watakaa viongozi mbalimbali wakati wa shughuli za kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa zitakazofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuanzia kesho Jumapili.
Ujenzi wa kibanda maalum ambacho kitatumika kuwekwa mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa kikiedelea kujengwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Moja ya mafundi akiendele na ujenzi wa kibanda kitakachotumika kuuweka mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Baadhi ya askari wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) wakiwa wamebeba choo cha kuhamisha ambacho ni sehemu ya maandalizi yanayaoendelea Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambako shughuli za kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa zitafanyika kuanzia leo kesho Jumapili hadi Jumanne
Sehemu ya askari wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) wakijenga hema kwa ajili ya maeneo ambayo yatatumika kwa shughuli mbalimbali wakati wa kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) wakiendelea na kufunga hema katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Moja uzio uliowekwa nje ya Uwanja Uhuru jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea siku ya kesho Jumapili ambako shughuli za kunza kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa zitafanyika.
Ujenzi wa kibanda cha kuweka mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa ukiendelea katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kazi ya kuandaa eneo la jukwaa kuu ambalo viongozi wa kitaifa watakaa ukiendelea Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa ngazi mbalimbali serikali pamoja na maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wakiangalia maendeleo ya ujenzi wa kibanda maalum ambacho kutatumika kuuweka mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Baadhi ya mafunzi wakiwa wamebeba kikoo ambacho kikitawekwa kwenye kibanda maalum kwa ajili ya kuwekwa mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Mabanda ya huduma ya kwanza yakiwa yamekamilika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya shughuli ya kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa viongozi mbalimbali wa Serikai kuhusu eneo ambalo mwili wa mzee wetu Rais mstaafu Benjamin Mkapa utakavyowekwa kwa ajili ya wananchi kutoa heshima zao za mwisho zitakazofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuanzia kesho Jumapili.Katikati ni Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanua jambo baada ya kufika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya eneo ambalo Rais mstaafu Benjamin Mkapa mwili wake utawekwa kwa ajili ya wananchi kutoa heshima ya mwisho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Idd(katikati) akitoa ufafanuzi baada ya kutembelea Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya maandalizi kwa ajili ya shughuli za kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.Wengine wanaomsikiliza ni viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Wazirii Mkuu Kassim Majaliwa(kulia).
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Jenerali Venancy Mabeyo akieleza jambo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine kuhusu namna ambavyo kibanda maalum ambacho kitatumika kuuweka mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa kitakavyokaa kwa ajili ya wananchi kutoa heshima zao za mwisho.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venancy Mabeyo akiwa na maofisa wengine wa jeshi hilo wakielezekana jambo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(wa pili kulia) na Makamu wa Pili wa Serikali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(wa tatu kushoto)baada ya kufika Uwanjwa Uhuru jijini Dar es Salaam kuangalia maandalizi ya kitaifa kwa ajili ya shughuli za kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(katikati) akisisitiza jambo kwa viongozi wa ngazi mbalimbali baada ya kufika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambako shughuli za maandalizi kwa ajili ya kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa zikiendelea.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Jenerali Venancy Mabeyo akiangalia mchoro wa kibanda maalum ambavyo kitakuwa baada ya kukamilika .Kibanda hicho ndicho kitakachokuwa na mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (aliyevaa suti) akitoa maelekezo kwa maofisa waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) baada ya kufika Uwanja wa Uhuru kuangalia maendeleo ya maandalizi kwa ajili ya shughuli za kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Hassan Abbas(kulia) akipata maelezo kabla ya kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu shughuli za kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa ambazo zinatarajia kuanza kesho Jumapili ambapo ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi wa Dar es Salaam kujitokeza uwanjani hapo kwa wingi ili kutoa heshima zao za mwisho kwa mzee wetu.
Baadhi ya waandaaji wa jukwaa kuu ambalo viongozi mbalimbali watakaa wakati wa shughuli za kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa zitakazofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuanzia kesho(Jumapili),Jumatatu na Jumanne
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiwa na viongozi wengine wakijadiliana jambo walipokuwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(kulia) akiwa na viongozi wengine wa Serikali wakishuka jukwaa kuu baada ya kufanyika kwa kikao ambacho kilikuwa na lengo la kujadili mwenendo wa maandalizi yanayoendelea Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya shughuli za kuaga mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiangalia jinsi ujenzi wa kibanda maalum ambacho kitatumika kuuweka mwili wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa kwa ajili ya wananchi kutoa heshima zao za mwisho.(PICHA ZOTE NA SAIDI MWISHEHE-MICHUZI TV)
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
VIONGOZI mbalimbali wakiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Baloz Seif Ali Idd na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wamefika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuangalia maendeleo ya maandalizi ya kitaifa ya eneo ambako shughuli za kuaga mwili wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa zitafanyika.
Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera,Bunge,Vijaana, Kazi ,Ajira na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika, Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi.
Pia Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dotto James na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sana'a na Michezo Dk.Hassan Abbas pamoja na maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania( JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Venancy Mabeyo aliyeambatana na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yakubu Mohamedi.
Kwa kukumbusha tu mwili wa mpendwa wetu,mzee Mkapa utaagwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuanzia kesho Jumapili, Jumatatu na Jumanne ambayo itakuwa ni siku ya kuaga kitaifa ambapo viongozi mbalimbali watahudhuria.
Akizungumza kuhusu maandalizi na hatua mbalimbali zinazoendelea hadi jioni ya leo Julai 25,2020 ,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ububakari Kunenge amesema kwamba maanda
Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, kama ambavyo nimeeleza hapo awali tutakuwa tunaendelea kuwahabarisha hatua mbalimbali ,hata hivyo kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa tano asubuhi katika uwanja huo kutakuwa na Misa ya kawaida na kisha wanananchi wataanza kutoa heshima zao za mwisho.
Pia amesema shughuli za kuaga zitaendelea na siku ya Jumanne kutakuwa na ibada ambayo itafanyika Kanisa la St.Immaculate Upanga jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja mpaka saa saba.Hata hivyo ameomba ushiriki wa wananchi kwa kufika kwa wingi kwa ajili ya kumuaga Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Hata hivyo amesema wananchi ambao watafika kwa ajili ya kuaga mwili wa mzee Mkapa kutakuwa na maelekezo yatakayokuwa yakitolewa kwa ajili ya kufanikisha shughuli hizo.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments