"Mkapa Alinifanya Nianze Kupiga Kura" - Shusho | ZamotoHabari.


Msanii wa nyimbo za Injili Tanzania Christina Shusho amesema moja ya matukio anayoyakumbuka kutoka kwa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa ni kupiga kura kwa mara yake ya kwanza na alivyotangaza kifo cha Baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere.



Akizungumza kwenye show maalum ya Friday Night Live Christina Shusho amesema

"Kikubwa ninachokikumbuka wakati wa uongozi wake kwa mara ya kwanza nikaanza kupiga kura kumbukumbu hiyo hainitoki nashukuru Mungu ni baraka, amefanya vizuri na tuna mengi ya kujifunza kutoka kwake, nakumbuka tena mwaka 1999 anatangaza kifo cha Baba wa Taifa kwa wakati huo ilikuwa ngumu kwa sababu tulikuwa tuna hofu ya kuingia mwaka 2000 maana tuliambiwa Yesu anarudi kutakuwa na mabomu, mlipuko na radi" ameeleza Christina Shusho 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini