Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (katikati) jana amesaini mkataba wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania na Mwenyekiti wa Kampuni ya Reli kutoka nchini China, Bw.Xie Zhixiang CRJE(East Africa) ambaye hayupo pichani .Jengo hilo litajengwa kwa muda wa miaka miwili, eneo la NCC Jijini Dodoma. Kushoto ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma na (kulia) ni Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Kevin Mhina.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Reli kutoka nchini China, Bw.Xie Zhixiang CRJE(East Africa) akisaini mkataba huo. Tukio hili limefanyika kwenye ofisi za Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania,Jijini Dar es Salaam.PICHA NA INNOCENT KANSHA - MAHAKAMA
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments