Msanii wa Kundi la Weusi Atangaza nia ya Kugombea Ubunge Jimbo la Kahama Mjini | ZamotoHabari.


Msanii wa Hip Hop nchini, kutoka Weusi Bonta Maarifa ametia nia ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge wa Jimbo la #Kahama Mjini ambapo ndipo anaishi na kufanya kazi.

Rapa huyo kutoka kundi la Weusi ametia nia ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kwa sasa kipo katika mchakato huo.

Bonta anakuwa msanii wa pili ya Hip Hop nchini kuweka wazi nia ya kugombea Ubunge baada ya Mwana FA ambaye aliweka wazi kama chama hicho (CCM) kitampitisha atagombea moja ya majimbo mkoani Tanga.

Ikumbukwe tayari wasanii kama Mr II ‘Sugu’ na Prof. Jay ambao walitamba sana kwenye muziki wa Hip Hop wameshakuwa wabunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini