Anaidaiwa kukimbia jikoni na kuchukua kisu kabla kumdunga mumewe kifuani na kumsukuma ukutani. Hisani.
Mwanamke aliyekamatwa na kufikishwa kortini baada ya kumdunga mumewe kisu tumboni wakikangangania simu amekiri makosa na kujitetea.
Mary Nduta alikiri kumdunga kisu mumewe Solomon Njoroge Maingi nyumbani kwao katika mtaa wa Mwiki, Kasarani Nairobi Julai 19.
Akizungumza mbele ya hakimu mkazi David Ndungu katika mahakama ya Mlimani, Nduta alieleza kuwa alimdunga kisu mumewe kama njia ya kujikinga baada ya kuzidiwa nguvu.
Mlalamishi, Solomon Njorogo Maingi anaendelea kupata matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta alikolazwa baada ya mkasa huo.
Njoroge alirudi nyumbani baada ya wiki mbili na mkewe kuanza kulalamika kuhusu jinsi mumewe wa kwanza alivyokuwa akimpa pesa nyingi kumshinda..
Njoroge alijua kuwa alikuwa katika mawasiliano na mume huyo na hivyo akataka kuona simu, hapo ndipo majibizano yalianza .
Nduta anaidaiwa kukimbia jikoni upesi na kuchukua kisu kabla kumdunga mumewe kifuani na kumsukuma ukutani.
Njoroge aliokolewa na jirani ambaye alifika upesi na kumtolea kisu hicho kifuani kabla kumkimbiza hospitalini kwa matibabu.
Mwanamke huyu alinaswa na maafisa wa polisi waliopata kisu pamoja na nguo ya kulala katika chumba chao cha kulala zikiwa na matome ya damu.
Nduta aliachiliwa kwa dhamana ya KSh 100,000 huku kesi yake ikisubiriwa kutajwa tena Agosti 4, 20202.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments