Mwanamuziki Wakazi Apinga Vikali COSOTA Kuhamishiwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo | ZamotoHabari.


Anza kusoma toka kwenye tweets za hapo juu. Kisha endelea hapa chini.

"Muziki una sura nyingi; SANAA, UTAMADUNI, BURUDANI, BIASHARA. Ni sahihi kwa muziki kusimamiwa na taasisi tofauti tofauti kulingana na sura husika. Sasa kuhamishia aspect ya Biashara chini ya Wizara ambayo inaweka emphasis on Utamaduni na Sanaa, kweli jamani?! "

"Cha kuchekesha sidhani hata kama 40% ya artist wamejiandikisha COSOTA."

"Alafu haya mambo ya kuchanganya Utamaduni (na Sanaa) juu ya Biashara, ndio yanadumaza ukuaji wa muziki wetu kibiashara. Biashara ya Sanaa imekuwa "global", "urban" na "cross-cultured". Ila sisi tunasingizia MAADILI ya Kitanzania kila siku, na kubana Artistic Expressions. It's Sad."

COSOTA hata iwekwe Wizara ya Fedha (and same goes for BASATA), hazitofanya vizuri kama hakutokuwa na fungu lililotengwa la kuwezesha utendaji wa taasisi hizo. Shida yetu sio Cosota na BASATA zipo wapi, bali ZINAFANYA NINI na KWA UWEZESHWAJI UPI. Je vipaumbele vyetu ni VIPI?! "
-"Ikumbukwe kuwa COSOTA haina ofisi mikoani na ndio maana pia tupo chini ya Wizara ya TAMISEMI, sababu Maafisa Utamaduni (Serikali Za Mitaa) ndio hutumika kukusanya Mirabaha yetu. Had COSOTA been properly funded, that wouldnt be the case. Wasanii vipaumbele vyetu ni vipi?! "

Ni vyema ku-address changamoto zetu za msingi kwanza, badala ya kufanya kitu cha "kisiasa" ambacho hakina manufaa direct ya kiuchumi kwa Wasanii.
• Malipo Hafifu
• Mirabaha
• Mfuko Wa Hifadhi
• Bima ya Afya
• Standardized Venue
• Music Academy
• Local Playlist
• Archives

Kiukweli, na hizi ni rai zangu; Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo imepewa majukumu mengi na makubwa sana kwa wao kuweza kufanikisha majukumu efficiently & effectively. Zivunjwe na kuwa "HABARI" na "MICHEZO NA BURUDANI" badala ya kuongeza aspect ya Biashara ndani yake.

Leo kuna sherehe ya kuhamishia COSOTA huko Wizara nyingine, ila ukweli ni kwamba hiyo sio solution hata kidogo. Wasanii hawajui vipaumbele vyao, na wengi wao hata hiyo move hawajui ina implications gani. Nimalizie tu kwa kusema...

"ULIMBUKENI WA WASANII NI MGODI WA WANASIASA" - @wakazi

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini