Niyonzima Aweka Kando Mkataba wa Yanga | ZamotoHabari.


LICHA ya kubakisha miezi miwili kabla ya mkataba wake kumalizika, kiungo nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima, amefunguka kwamba ameamua kuuweka kando mkataba wake mpya na timu hiyo.

Niyonzima amesema ameamua kufanya hivyo kwa kutaka kwanza wamalize masuala ya ligi kisha aanze mazungumzo na mabosi wake huku akiweka wazi kuwa kama ikishindikana anaweza kuondoka.

Kiungo huyo Mnyarwanda alitua Yanga kipindi cha dirisha dogo Desemba, mwaka jana akitokea AS Kigali ya kwao na kuanguka saini ya miezi sita.

Mnyarwanda huyo ameliambia Championi Jumatatu, kuwa licha ya mkataba wake kwenda kumalizika, lakini kwa sasa ameliweka kando suala hilo na kutaka kwanza kumaliza mechi za Ligi Kuu Bara ambayo ilitarajiwa kumalizika jana Jumapili.

Kiungo huyo ameongeza kuwa, baada ya hapo atakaa na kuzungumza na mabosi wake na kuwapa vile anavyovitaka ambapo kama itashindikana anaweza kuondoka.

“Kwa sasa hivi naona bora timu icheze tumalize vizuri mechi iliyobaki kwenye ligi kisha baada ya hapo mambo mengine yatakuja.

“Mimi kama mchezaji mkataba wangu unaenda kumalizika keshokutwa imebaki kama miezi miwili tu lakini siwezi kuzungumzia kwa sasa kwa sababu nataka kumaliza masuala ya ligi.

“Ikiisha nitaongea na viongozi na kuwapa mahitaji yangu kama mchezaji na nitazungumzia juu ya kubakia lakini ikishindikana nitaondoka,” alisema kiungo huyo.

MUSA MATEJA NA SAID ALLY

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini