Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mikumi (Chadema), Joseph Haule, maarufu kwa jina la Profesa Jay amemkaribisha nyumbani Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Profesa Jay amesema wapi tayari kumpokea kesho uwanja wa ndege na kwamba atafika kabla ya majira ya saa 7:20 mchana.
Kiongozi huyo aliandika ujumbe huu katika ukurasa wake wa Twitter kuwa “Karibu sana nyumbani shujaa Tundu Lissu, tupo tayari kukupoke kesho pale Airport, Binafsi nitakuwepo mapema sana kabla ya saa 7:20 mchana utakapotua Airport. Kesho tukutane airport,”.
KARIBU SANA nyumbani Shujaa TUNDU LISSU, Tupo tayari kukupokea kesho pale Airport , Binafsi nitakuwepo mapema sana kabla ya saa 7: 20 Mchana utakapotua AIRPORT.— Joseph L. Haule (@ProfessorJayTz) July 26, 2020
Kesho Tukutane AIRPORT🙏🏻🙏🏻 pic.twitter.com/LbUQIxd4Cm
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments