Na MWAMVUA MWINYI,PWANI
RANCHI ya Ruvu ,Bagamoyo mkoani Pwani, imeongeza mapato yake kutoka milioni 50 kwa mwezi hadi kufikia makusanyo ya milioni 100 .
Aidha imefanikiwa kuokoa kiasi cha sh .milioni 20 zilizotokana na upunguzaji wa watumishi wasio wa lazima ,kujenga miundombinu imara isiyoongeza gharama za kiutendaji na kupunguza matumizi yasiyo ya ulazima.
Kauli hivyo imetolewa na meneja wa Ranchi ya Ruvu, Elisa Binamungu ,alipokuwa anaelezea mafanikio ,maboresho na changamoto katika kipindi cha miaka mitano .
"Fedha hii ya mapato imeongezeka kutokana na mauzo ya nyama ,ngozi ,tozo za vitalu na wanyama wadogo " anasema Binamungu .
Aidha anaeleza, Ranchi ya Ruvu ilikuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi baina yake na wananchi ,uvamizi wizi wa mifugo ya Ranchi na ufugaji holela hali ndani ya kipindi cha miaka mitano ambapo changamoto hizo zinaelekea kuwa historia.
";Hii hali ilisababishwa na tatizo la kutokuwa na mipaka na alama zinazoonyesha eneo la Ranchi ambapo baada ya kuwekwa alama hizo tatizo la migogoro hiyo limepungua ."
Binamungu anasema, kuweka alama za kudumu kutenganisha maeneo ya Ranchi na jamii kumesaidia kupunguza migogoro ya ardhi sanjali na kutenga eneo la hekta 20,000 ambalo limepimwa vipande vya hekta 500 na kupatikana vitalu 40 vinavyotumika kwa wafugaji wadogo ili kupunguza pia mifugo holela mkoani hapo .
Anaeleza ,wanahamasisha kuanzia ngazi ya kijiji ,kata lengo mifugo inayoingia ndani ya Ranchi iingie kwa utaratibu maalum ikiwa ni pamoja na kila heka moja mfugaji anailipia tozo 3,500 kwa mwaka"
Hata hivyo ,anaelezea kwamba ,nyama wanauza ya kiwango ,kilo moja 7,000 ,wana duka la nyama katika Ranchi na jingine Dar es salaam ,wanauza kwa wateja mmoja mmoja ,jumla na kwa wasambazaji kwa wenye mahitaji .
Binamungu alitaja malengo yao kuwa ni kuboresha miundombinu zaidi ili kujiimarisha ,kujenga machinjio ya kisasa .
Lengo jingine ni kuongeza uzalishaji wa mifugo ya maziwa kwani wamegundua kuna fursa kubwa ya uuzaji maziwa baada ya soko kupanda la maziwa huku kukiwa na upungufu wa maziwa .
Tunahitaji kuanzisha mashamba darasa ,hii ni Ranchi kubwa mashamba darasa yatasaidia kuwaongezea ulewa wafugaji kufuga na kuondokana na uchungaji ,wa kufuga kiholela ,kienyeji ,ni wajibu wao kufuga kisasa .
Binamungu anatoa wito kwa wafugaji kujiunga vikundi vidogo ili kuomba maeneo katika Ranchi hiyo ili pia kupunguza migogoro na wakulima kwenye maeneo yao .
Ranchi ya Ruvu ,ilianza mwaka 1957, kwasasa ina jumla ya wafanyakazi 43, mifugo ya ng'ombe 1,500 ,mbuzi 400 na kondoo 780.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments