Sababu za Jokate ‘Kutoolewa’ Zaanikwa | ZamotoHabari.



DAR: Baada ya Rais Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’ kuwashangaa watani zake Wazaramo kwa kushindwa kumuoa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Urban Mwegelo (33) ilhali hana mume, sababu za mrembo huyo kutoolewa zimeanikwa.

KAULI YA JPM

JPM alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kisarawe mkoani Pwani, mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa Kibamba hadi Kisarawe uliogharimu shilingi bilioni 10.6 za Kitanzania.


Alisema; “Hata Mkuu wa Wilaya wa hapa (Jokate) amefanya kazi nzuri katika kuondoa zero. Hapa kulikuwa na zero nyingi sana, ninachowashangaa watani zangu Wazaramo hawajamuoa, lakini mmeshindwa kumuoa mnamuangalia tu, ndiyo shida ya Wazaramo, saa zingine mnashindwa mambo…”

KWA NINI HAOLEWI?



Kwa mujibu wa wataalam mbalimbali wa elimu ya saikolojia waliozungumza na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, mara kwa mara kumekuwa na tabia ya wanaume kutamani kuwa kwenye uhusiano na wanawake warembo kama Jokate ambaye ni mshindi wa pili katika Shindano la Miss Tanzania mwaka 2006.

UZURI UNAMPONZA

Wataalam hao wanataja kigezo cha uzuri wa sura na umbo kuwa, vimekuwa vikitumiwa na wanaume kuogopa kuoa wanawake wazuri kama Jokate wakiamini hawawezi kuwahudumia, hivyo wanawake wengi wanaponzwa na uzuri wao.

“Hii imewaacha mabinti wengi warembo wa sura na maumbo katika maumivu makali sana ya mioyo yao.“Wengi badala ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwajaalia uzuri wa sura na maumbo namba nane, wamejikuta wakikata tamaa,” anasema mmoja wa wataalam hao.



WENGI WACHEZEAJI (PLAY BOYS)

Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu ulibaini kwamba, katika kipindi tulichonacho, kumekuwa na wimbi la wanaume wengi ambao ni wachezeaji wa wanawake (play boys), jambo ambalo Jokate amekuwa nalo makini.“Hakuna jambo wanalochukia wanawake kama wakijua wanachezewa. Mwanamke yupo tayari awe ‘singo’ kama Jokate ili tu asichezewe,” anasema mtaalam mwingine.



MR RIGHT HAJATOKE

AInasemekana baadhi ya wanawake wazuri, wasomi na wenye vyeo kama Jokate, wanaamini kwamba wanaume wanaowasogelea ni kwa ajili ya kujifurahisha kimapenzi tu na baada ya hapo watawakimbia, hivyo kuwa makini mno juu ya nani wawakabidhi mioyo yao.Inasemekana kwamba, katika hali kama hii, wengi wamekuwa wakisubiria kuwapata mwanaume sahihi (Mr Right).



Inaelezwa kuwa, tabia hii ya kusubiria Mr Right atokee, imekuwa ikiwafukuza wanaume wanaojitokeza kwa kunyimwa ushirikiano.



UBIZE WA JOKATE

Inafahamika kwamba, Jokate ni mkuu wa wilaya pekee mwenye majina au vyeo mbalimbali nchini Tanzania. Kwa ufupi tu ni kwamba, mbali na ukuu wa wilaya, Jokate ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kidoti, mwanamitindo, mfanyabiashara, mshereheshaji, mwigizaji, mwimbaji, mtangazaji wa televisheni na mengine mengi, hivyo wanaume wanaamini atakuwa bize zaidi na mambo hayo kuliko kuhudumia ndoa na familia.Mbali na hayo, Jokate amekuwa bize mno akitekeleza kampeni na miradi mbalimbali.



Kuna kipindi alikuwa bize mno na kampeni yake ya Tokomeza Zero Kisarawe, ujenzi wa shule maalum ya wasichana (Jokate Girls) na kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Kisarawe.



Pia amekuwa akifanya kazi kubwa mno ya kuhamasisha maendeleo wilayani Kisarawe hasa kupitia kilimo akiwaaminisha wananchi kuwa wanapaswa kulilisha Jiji la Dar kwa vyakula mbalimbali na kujipatia kipato.Majukumu yote hayo, jumlisha na kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ambapo anasimamia usalama wa wananchi wake kwenye ukanda huo.



JOKATE ANAOGOPWA

Kwa mujibu wa mtaalam mwingine wa saikolojia, wanawake wa aina ya Jokate; yaani wazuri wa sura na umbo, wenye vyeo na elimu kubwa, wamekuwa wakiogopwa na wanaume.



Kwa hiyo, kinachotokea ni kwamba, wanaume wakishapata bahati ya kufaidi penzi mara moja au mbili kwa wanawake wa sampuli hii, huwakimbia tena kwa kasi wakihofia kukamuliwa kiuchumi, ingawa mara nyingine hofu yao hii huwa siyo ya kweli.



Baadhi ya wanaume waliotoa maoni yao kwenye hili juu ya kuoa wanawake sampuli ya Jokate, wanawake wa aina hii wanapendwa kwani mwanaume anayetembea naye hujihisi sifa sana, hususani anapoonekana na wanaume wenzake, yaani kama vile timu ndogo iliyopata nafasi kucheza katika Kombe la Dunia.



“Si unajua tena wanaume wanavyopenda kujionesha wanapokuwa na vifaa (wanawake wazuri) mbele ya macho ya wanaume wenzao?



“Lakini unapofikiria kuishi na mwanamke kama huyu kama mume na mke, lazima utaingiwa na hofu ya kuelemewa au kujihisi kutokuwa salama maana kila mwanaume anammezea mate,” anasema Innocent Milanzi, mkazi wa Mbagala jijini Dar na kuongeza;



“Hapa ishu inakuwa ni kuibiwa na wanaume wenye kisu kikali (pesa).”Wanaume wengine waliozungumza na mwandishi wetu juu ya mjadala huo, walisema, wanawake kama Jokate ni wa gharama mno na siyo rahisi kuwaweka mjini na kuhakikisha wanaishi maisha yao ya kawaida kama huna mkwanja wa kueleweka au cheo kikubwa kuliko chake.



Hata wale wanaume wachache ‘wanaomiliki’ wanawake wa sampuli ya Jokate, wameeleza jinsi wanavyohisi wanatumia pesa nyingi na yamkini zaidi ya wanavyojiweza.



IDADI YA WATOTO

Wengine walikwenda mbali zaidi na kueleza kwamba, hata unapotaka kuzaa na mwanamke wa sampuli ya Jokate, basi yeye anataka mtoto mmoja au wawili tu, akiogopa asije kuharibu umbo lake, tofauti na kiu ya mwanaume ya kupata watoto zaidi ya wawili.



Katika uchunguzi huu na ukiangalia hali halisi ya maisha ya kila siku, tena katika jamii tofauti, utagundua kwamba wanaume kiu yao siyo kuoa wanawake warembo, wenye vyeo, umaarufu na pesa, bali wanaume wanapotaka kutafuta mke wa kuoa, wanaangalia tabia na haiba zilizojificha.



SIFA ZA MWANAUME WA KUMUOA JOKATE

Katika intavyu na gazeti hili alipotembelea ofisi za Global Group miezi kadhaa iliyopita, Jokate aliulizwa juu ya ishu ya kuolewa na sifa za mwanaume wa kumuoa ambapo alifunguka;“Kiukweli natamani kuwa na familia yangu, natamani kuwa na mume wangu na watoto wangu na naamini Mwenyezi Mungu akijaalia nitakuwa nao.



“Ni kitu ambacho ningependa kuwa nacho, God’s time is the best.“Kwa sasa ningependa kuwa na mtu ambaye ni mwelewa sana kwa sababu kazi za uongozi si lelemama, awe Mcha Mungu kwa sababu changamoto ni nyingi, bila kuwa na Mungu huwezi kukabiliana nazo kwa nguvu zako mwenyewe.”



Jokate aliteuliwa na JPM kushika wadhifa wa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe tangu mwaka 2018 ambapo ameifanya wilaya hiyo kuwa gumzo kutokana na uchapakazi wake akilenga kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi wake.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini