Saniniu Laiza: NAWAAMINI WATAALAM WA GST | ZamotoHabari.

 mchimbaji mdogo wa Madini ya Tanzanite  Bw. Saniniu Laiza akisaini kitabu mara baada ya kufika katika banda la GST katika maonesho ya 44 ya kibiashara katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
mchimbaji mdogo wa Madini ya Tanzanite  Bw. Saniniu Laiza akiwa katika  Picha ya pamoja
Na Samwel Mtuwa - DSM.
Leo Julai 12, 2020 , mchimbaji mdogo wa Madini ya Tanzanite, Saniniu Laiza ameipongeza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwa Utafiti za uhakika inazofanya katika sekta ya Madini nchini.

Laiza amesema hayo leo alipotembelea Banda la GST katika maonesho ya 44 ya Sabasaba yanayotarajiwa kufungwa kesho.

Akizungumza na Daktari Mussa Budeba ambaye ni Mtendaji Mkuu wa GST wakiwa katika banda hilo,  mchimbaji Laiza aliwapongeza wataalam wa GST kwa juhudi kubwa wanazofanya kwa wachimbaji wadogo wa Madini kwa kuwaelekeza juu ya uchimbaji bora na wenye tija kwa uchumi.

Sambamba na pongezi hizo kwa GST Mchimbaji Laiza alipata fursa ya kupiga picha ya pamoja na wataalam ikiwa ni ishara ya kuonesha kuwa ametembelea Banda hilo.

Mapema baada ya kumaliza kuzungumza na mchimbaji Laiza, Dk. Budeba  alizungumza na vyombo mbalimbali vya Habari juu ya majukumu ya GST 

Mnamo Juni 24, 2020 Serikali kupitia Wizara ya Madini ilitangaza kupatikana kwa madini mawili ya Tanzanite moja likiwa na kilogram 9.2 na lingine likiwa na kilogram 5.8 yaliyochimbwa na Mchimbaji huyo.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini