Soko la nyama lipo nchini la kutosha. | ZamotoHabari.


*Bodi ya nyama yasisitiza ulaji nyama.


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Katibu wa Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi -Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema soko la nyama lipo nchini la kutosha na kuwataka watanzania kujenga viwanda


Akizungumza katika Banda la Bodi  ya Nyama Tanzania (TMB) katika maonesho ya Biashara Kimataifa Profesa Ole Gabriel serikali imeweka mazingira bora ya uwekezaji katika sekta ya mifugo kwa ajili nyama.


Ametaka Msajili wa Bodi ya Nyama kuwasaidia wenye viwanda vya nyama kupata mikopo katika taasisi za fedha.

 Nae Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Dkt Imani Sichalwe  ameitaka Jamii kujenga mazoea ya kula nyama kwa wingi kwa sababu huleta vichocheo vya homoni zinazosadia uzazi.

Sichalwe amesema  kila mtu anatakiwa  kula  nyama kilogram 50 kwa mwaka ili kujenga afya bora na kupata protini nyingi katika mwili

Amesema ulaji nyama unaokidhi viwango unasaidia jamii kuondoka na tatizo la magonjwa mbalimbali ikiwamo ukosefu wa uzazi.

"Nyama ni muhimu kwa afya bora ili mtu apate  protini zinazohitajika ni lazima ale kilogram 50 kwa nwaka itamsaidia kumuepusha na maradhi,"alisema Sichalwe.

Alisisitiza kuwa  ulaji wa nyama ni muhimu sana katika mwili wa binadamu kwa sababu usaidia kutegeneza mifupa,Ujenzi wa akili na kuongeza  mwili  na kuongeza homoni mbalimbali.

Amesema kwa watu ambao awali nyama wamekuwa wakikosa vitu vingi katika mwili wao kutokana na kutokula nyama.

"Ubora wa protini ulioko katika nyama ni mkubwa zaidi kuliko ubora mwingine ambao unakosekana katika protini nyingine"alisema Dkt Sichwale

Akizungumza Maonesho ya Sabasaba 77 Dkt Sichwale amesema wamekuwa wakionesha kazi mbalimbali ambazo zimekuwa  zikifanywa na bodi  hiyo ikiwemo  kutoa mafunzo katika mmyololo mzima wa thamani wa nyama.

"Tukizungumzia suala la  nyama Bora  inatakiwa lianzie katika mashamba ambako kuna uchaguzi wa mbegu ,ulishaji mifungo pamoja na usafirishaji"amesema Dkt Sishwale.

Amesema pia wamekuwa wakiamasisha wananchi juu ya  ujenzi wa Viwanda vya kisasa ikiwemo machinjio pamoja na kujua namna ya kusafirisha vyema mifungo na nyama.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza katika Banda la Bodi ya Nyama alipotembelea maonesho biashara kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Dkt. Imani Sichalwe  akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na utendaji wa udhibiti wa nyama nchini katika maonesho biashara kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar Salaam.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini