TANESCO YATOA ELIMU KWA WACHIMBAJI DHAHABU MGODI WA NHOLI WILAYANI BAHI JUU YA MATUMIZI BORA YA UMEME | ZamotoHabari.

Wachimbaji wadogowadogo wa dhahabu katika mgodi wa Nholi wilayani Bahi kupatiwa nishati ya umeme ndani ya miezi sita ili kuongeza uzalishaji katika mgodi huo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mhandisi Mtafiti Aurea Bigirwamungu wakati wa kutoa elimu kwa wachimbaji wadogowadogo na wakazi wa kata hiyo kwa ajili ya matumizi bora ya umeme.
 Mhandisi Bigirwamungu amesema kuwa mradi wa kuwafikishia nishati ya  umeme wakazi hao utatekelezwa ndani ya miez sita ili kurahisisha shughuli za wajimbaji hao hasa katika uchenjuaji wa dhahabu na shughuli nyingine katika mgodi huo.

Aidha Mhandisi Bigirwamungu amesema kuwa wachimbaji hao shughuli zao nyingi zinahitaji nishati ya umeme ili kuongeza uzalishaji katika ujimbaji wa dhahabu ambapo nishati hiyo itaweza kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
“Ninaimani kubwa  ndani ya miezi sita mradi huu  utatekelezwa na kukamilika hivyo wakazi wa hapa watanufahika na kuongeza chachu katika uzalishaji na maendeleo yao ” ameweka wazi Mhandisi Bigirwamungu.

Lakini pia Mhandisi Bigirwamungu amesisitiza kuwa baada ya elimu hiyo wachimbaji hao wahakikishe wanatumia vifaa vilivyo bora hasa ambavyo havitumii umeme mwingi , lakin pia kuwa na matumizi mazuri ya umeme kila baada ya matumizi kuzima umeme huo.

Naye Afisa Masoko Adelina Lyakurwa ametoa wito kwa wakazi hao kuchangamkia fursa ya kupata nishati ya umeme ili kuongeza uzalishaji katika shughuli zao za uchimbaji.

“Hivyo basi taratibu za kufanikiwa kupatiwa umeme ni kuhakikisha unapata fomu ya kuomba kupatiwa umeme, ukisha jaza fomu hiyo isainiwe na mkandarasi alafu irudishwe TANESCO na fanya kutandaza nyaya katika nyumba yako muda ukifika basi wewe ni kufungiwa umeme” amebainisha Lyakurwa.

Aidha Lyakurwa ameongeza kwa Nishati hii ya umeme kwa wakazi hao wataunganishiwa nishati ya umeme kwa shilingi 27,000 tu.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano Huduma kwa Wateja TANESCO Dodoma Mariam Juma ameweka wazi kuwa lengo la kuwasogezea nishati ya umeme wakazi hao ni kuhakikisha wanatumia nishati hiyo kuchenjua dhahabu na shunguli nyinginezo katika mgodi huo ili kuongeza uzalishaji wa dhahabu katika mgodi huo na kuleta maendeleo kwa ujumla.

Pia Mariamu amewashukuru wakazi wa kata hiyo kwa mwitiko waliyowapa na kusema kuwa elimu waliyopatiwa  itakwa na manufaa kwao na kuleta tija kwao.

Kwa niaba ya wachimbaji na wananchi wa kata hiyo Meneja mgodi Kulwa Limbu ametoa changamoto ya wachimbaji hao kuwa wamekuwa wakitumia dizeli katika shughuli zao za uzalishaji wa dhahabu ambayo imekuwa ikuuzwa kwa bei ghali na kusababisha shughuli za mgodini kutotekelezwa ipasavyo.

“Sisi tuko tayari kutumia nishati ya umeme hivyo nitoe wito kwenu watendaji wa TANESCO kuwa mradi huo uweze kukamilika ndani ya muda mliosema ili tuweze kunufaika na mradi huo kwa kuongeza uzalishaji ” ametoa rai
 Mhandisi Mtafiti TANESCO Aurea Bigirwamungu akikagua baadhi ya mitambo ya wachimbaji wadogowadogo wa Dhahabu wa Mgodi wa Nholi wilayani Bahi .
 Mhandisi Mtafiti wa TANESCO, Aurea Bigirwamungu akizungumza   wakati wa kutoa Elimu kwa Wachimbaji wadogowadogo wa Dhahabu katika Mgodi wa Nholi uliyopo wilayani Bahi  juu ya matumizi bora ya Umeme.
 Afisa Masoko TANESCO,Adelina Lyakurwa akizungumza na wachimbaji wadogowadogo wa Dhahabu katika Mgodi wa Nholi(hawapo pichani) uliyopo wilayani Bahi  wakati wa kutoa elimu juu  ya matumizi bora ya Umeme.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini