Tapeli Hush Puppi na Wenzake 12 Wakabithiwa Mikononi Mwa FBI Marekani... | ZamotoHabari.

Mwanamtandao maarufu wa nchini Nigeria @hushpuppi na wenzake 10 wamekabidhiwa kwenye mikono ya Shirika la Kijasusi (FBI) na kufikishwa nchini Marekani, eneo ambalo wanadaiwa kutenda uhalifu wao. Zoezi hilo limefanywa na polisi wa Dubai ambao waliwakamata mapema mwezi uliopita.

Hushpuppi na wenzake hao walitiwa nguvuni na kikosi kazi cha polisi wa Dubai kwa ushirikiano na Polisi wa Kimataifa kwenye operesheni iliyopewa jina la Fox Hunt 2. Wanatuhumiwa kwa makosa kadhaa ikiwemo Utapeli, Utakatishaji fedha, Udukuzi, Wizi kwenye taasisi za Kibenki na Utapeli wa mtandaoni ambapo wanadaiwa kudukua barua pepe na tovuti za mabenki kisha kujihamishia fedha kwenye akaunti zao.

Mbali na kuwakuta na pesa taslimu kiasi cha TSH. Bilioni 92.7, Hushpuppi na genge lake wanadaiwa kutapeli takribani Trilioni 1 za Kitanzania kwa watu milioni 1.9 duniani. Pia wanatuhumiwa kufanya utapeli wa kuhamisha fedha kiasi cha TSH. Bilioni 81 za ununuzi wa vifaa vya Upumuaji 'Ventilators'' kutoka Serikali ya Marekani kwenda kwa raia wake waishio Afrika.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini