TASAC YATARAJIA KUTOA GAWIO KWA SERIKALI ZAIDI YA SH. BILIONI 20. | ZamotoHabari.


*Yaweka mikakati ya kwenda kwa kasi kwa kuongeza katika pato la taifa

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema kuwa kwa mwaka huu linatarajia kutoa gawio kwa Serikali la zaidi ya Sh. Bilioni 20.

Akizungumza na waandishi wa alipotembelea  Banda la Shirika hilo katika maonesho ya 44 ya  Biashara Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam Mkurugezi Mkuu wa TASAC Emmanuel Ndomba amesema utoaji wa gawio hilo linatokana na kuweka mikakati mbalimbali katika ukusanyaji wa mapato.

Ndomba amesema wamekuwa wakifanya majukumu mbalimbali yakiwamo ya uhakiki wa mizigo, uangaliaji na uhakiki wa nyaraka zote za mizigo inayokuja Tanzania kwa njia ya meli, na kuongeza kuwa kazi hizo ndizo zimekuwa zikiwangizia fedha zinazowawezesha kulipana mishahara na kutoa gawio kwa Serikali.

Aidha TASAC imetangaza nafasi 60 za ajira katika shirika hilo hivyo limewaomba vijana kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi hizo ili waweze kufanya kazi na kuinua uchumi wa nchi

"Tumeanza muda mfupi 2017 lakini mwaka jana tulitoa gawio kwa Serikali kiasi cha Sh. Bilioni 10 na mwaka huu tunatarajia kuchangia mara mbili zaidi ya tulivyofanya mwaka jana, pia tumefanikiwa kutengeneza ajira kwani tumeshatangaza ajira 60 kwa vijana ambao wakipatikana watafanya kazi katika sekta zote tulizonazo," amesema

Ndomba amesema  kwenye uchumi endelevu lazima kipengele cha usajili na kuongeza kuwa asilimia 90 ya mizigo yote inayosafirishwa duniani inapitia baharini.

Amesema Tanzania tuna habati kwani tuna eneo kubwa la bahari na Serikali ilifanya vema kuwa na chombo hiki cha TASAC ambacho kinahakikisha kwamba ufanyaji wa biashara katika meli unalinda pia mazingira na usalama yanalindwa, jambo hilo tumelifanya kwa juhudi na  tumekuwa tukitoa elimu kwa watumiaji na wasafiri kuhusu nini wafanye wanapokuwa katika vyombo hivyo.

Kuhusu ajira, amesema ajira walizozitangaza ni kwa wale vijana wenye ujuzi, uzoefu na utaalamu wa kuondoa mizigo na bidhaa  na kuongeza kuwa watakaopatikana watasambazwa katika sehemu zote wanazozifanyia kazi ambazo ni mipaka, viwanja vya ndege na bandarini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli nchini (TASAC) Emmanuel Ndomba akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Tasac Maonesho ya 44 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini