TCRA Yavipiga Faini Vyombo vya Habari Sita vya Utangazaji Milioni 28 | ZamotoHabari.


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -TCRA imevitoza faini vituo  vya utangazaji  jumla ya shilingi Millioni 28 kwa kosa la ukiukaji wa kanuni za Maadili ya  utangazaji.

Vituo vilivyotozwa faini ni pamoja na Clouds Fm, Duma Tv,  East Africa Radio, Global Tv, Sibuka Televisheni pamoja na Star Tv ambapo kila kituo kimetozwa faini kulingana na kosa lake

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati akitoa hukumu hiyo Makamu Mwenyekiti kamati ya Maudhui Joseph Mapunda amesema kabla ya hukumu hiyo waliitwa wahusika na kamati ya maudhui na kujiridhisha kwa vituo hivyo kwa  makosa  ya ukiukaji wa kanuni za utangazaji.

Mapunda amesema kua katika hukumu hiyo kituo cha Duma Tv kimefungwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Leo ambapo faini yake shilingi milioni saba.

Aidha emefafanua kua kwa watu wasioridhika na uamuzi huo wanaweza kukata rufaa kwa siku ishirini na moja kuanzia leo.

Faini hizo kama ifuatavyo Clouds Intertainment Radio sh.milioni 5,Duma online TV sh.milioni 7,East Africa Radio sh.milioni 3,Global Tv sh.milioni 7,Sibuka Televisheni  sh.3.Star Tv sh.milioni 5.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Joseph Mapunda akisoma hukumu kwa vyombo sita vya habari vya utangazaji kwa kukiuka maudhui ya utangazaji.
OPEN IN BROWSER


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini