Uchebe Asema Picha Alizoonyesha Shilole ni Kipigo cha Siku Nyingi na Hajalala Nyumbani Siku Mbili | ZamotoHabari.


Ashrafu Sadiki maarufu kwa jina la Uchebe amesema picha ambazo amitupilia Mwanamuziki Zuena Mohammed maarufu kama Shilole katika mitandao ya kijamii akilalamikia kupigwa ni za muda mrefu kabla ya ndoa yao.

“Sijui kwa nini kafanya hivyo wanawake wasanii mtihani sana hizo picha ni za muda mrefu sana…. Hata kumuoa sijamuoa enzi hizo kipindi hicho Shilole hajaacha mambo yake,”

“Sio kwa sababu sina hela simtimizie mambo mengine ndio anidharau mimi eti vile ana hela viongozi wanamjua sio sahihi,”alisema Uchebe.

Alisema suala la kudai amempiga siku mbili sio taarifa za kweli kwani hajalala nyumbani siku mbili na hajui alipolala.

“Acha tu huyu hajalala nyumbani siku mbili sijui alipo nampiga wapi ikifika wakati nitaongea yote,” alisema Uchebe

Alipohojiwa kama Shilole amedai talaka au la alijibu “Hayo tumuachie Allah mwenyezi Mungu ndio mwingi wa rehema tumuachie!,”

 Jana Shilole amevunja ndoa yake na Uchebe ikiwa ni baada ya miaka miwili ya wawili hao kufunga ndoa kwa kile alichodai kupigwa mara kwa mara na mume wake.

Shilole  alitangaza uamuzi huo kupita ukurasa wake wa Instagram na kuomba radhi kwa umma kutokana na kushindwa kusema juu ya manyanyaso anayopita kwenye ndoa yake.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini