Ugomvi wa Mali: Kanisa Lashambuliwa, Watano Wauawa | ZamotoHabari.



Polisi Afrika Kusini wamesema watu watano akiwemo mlinzi wa Kanisa la ‘International Pentecostal Holiness’ wamepigwa risasi na kuchomwa moto hadi kufa baada ya washambuliaji kuvamia Kanisa hilo na kuteka waliokuwemo

Polisi wamefanikiwa kuwaokoa waliotekwa na kuwakamata takriban watu 40 na kuzuia bunduki 16, bastola 13 na bunduki za rasharasha 5. Inasemekana uongozi wa Kanisa hilo umekuwa katika ugomvi tangu aliyekuwa kiongozi wa Kanisa alipofariki 2016

Kulingana na msemaji wa kikosi cha Polisi cha taifa, Brigedia Vish Naidoo, kundi lililoshambulia lilifahamisha kundi lililokuwa ndani ya kanisa kwamba wanakuja kutwaa udhibiti wa jengo la kanisa

Ifahamike kuwa Mwaka jana, fedha za kanisa takribani 15,206,007,982 zilipotea na hazijulikani zilipo

Idara ya Polisi ya Afrika Kusini imesema miongoni mwa waliokamatwa ni Maafisa wa Polisi wa idara hiyo, maafisa wa kikosi cha Jeshi la Ulinzi, maafisa Polisi wa mji wa Johannesburg pamoja na maafisa wa idara ya huduma ya Magereza



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini