Mkuu wa Chuo Cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi akitoa mafunzo kwa wataalamu na makufunzi wa vyuo malimbali hapa nchini kuhusu kwenda kidijitali katika masuala ya manunuzi na Ugavi
WATAALAM Wa masuala ya Ugavi nchini waaswa kuendana na ukuaji wa teknolojia nchini, na kuendana na dunia ya kidigitalj ilivyo, mifumo yao iende kidijitali na wafanye biashara kidijitali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es. Salaam leo, wakati wa kufungua mafunzo ya Teknolojia ya kidijitali katika Mnyororo wa Manunuzi na Ugavi, Mkuu wa Chuo Cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi, amesema kuwa wasioendana na teknolojia watapitwa.
"Washiri wa mafunzo haya lazima nao kuendana na mabadiliko nao wawe na uelewa wa dunia ya kidijitali ilivyo lazima mifumo yao iendane na teknolojia wafanye biashara kidijitali, lasivyo watapitwa na maendeleo yanayokuja duniani." Amesema Profesa Ngowi.
Amesema kuwa zamani ilikuwa lazima uwe na bohari kubwaa lakini baada ya kwenda kidijitali sio lazima kuwa na bohari kubwa ili uweze kufanya biashara
Hata hivyo Profesa Ngowi amesema kuwa wataalamu wa masuala ya ugavi wajaribu kwa kila namna ili kuendana na mapinduzi makubwa ya teknolojia yanayofanyika duniani kote.
Licha ya kwenda kidijitali katika masuala ya ugavi chuo kikuu cha mzumbe kampasi ya Dar es Salaam hawapendi mtu yeyote aachwe katika dunia ya kidijitali wa ugavi na wapo tayari kutoa mafunzo ya teknolojia ya kidijitali ili kuendana na malengo ya milenia ya hakuna mtu ataachwa nyuma katika nnyororo wa Ugavi.
Kwa Upande wake Mwakilishi mkazi wa shirika la Kuhne Foundation, Betrice Miru, amesema kuwa shirika la Kuhney wanafanya kazi ya kusaidia walimu pamoja na wataalamu wa masuala ya mnyororo wa manunuzi na ugavi hapa nchini.
Amesema kuwa wameshafanya semina mbalimbali kwaajili ya kuwajengea uwezo wadau wa ugavi kwani kumekuwa na mafanikio makubwa kwani washiriki wanajitokeza kwa wingi.
Betrice amesema kuwa wataalamu wa masuala ya ununuzi na ugavi wameweza kutoa changamoto wanazozipitia ili kuweza kuandaa mafunzo mengine na kuangalia ni nini kinahitajika kuendana na dunia ya ununuzi ugavi inavyoelekea.
"Katika kushirikiana na Chuo Kikuu Cha Mzumbe tumeona ushiriki umekuwa mzuri kwani tumepata washiriki wengi na mafunzo yanaonesha mlengo chanya katika masuala mazima ya myororo Manunuzi na Ugavi." Amesema Beatrice.
Kwa upande wa Mratibu wa Mradi wa Kuhne na chuo kikuu cha Mzumbe, Daktari, Omary Swalehe amesema kuwa mafunzo haya yanatolewa kwa taasisi za umma na taasisi binafsi ili kuweza kuboresha shughuli za Mnyororo wa manunuzi na ugavi hapa nchini.
"Tumeleta mafunzo ya teknolojia ya kidijita katika mnyororo wa Manunuzi na ugavi kwa sababu dunia ndiko inakoelekea."
Manunuzi na ugavi sio visiwa nayo inaendana na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia. Amesema Dkt. Omary.
Amesema wamelenga kuwawezesha wataalamu kupata elimu ya kidijitali katika masuala ya manunuzi na ugavi ili kuweza kuboresha ufanisi katika kazi zao.
Dkt. Omary ametoa wito kwa wanamanunuzi wa ugavi kushiriki fursa za mafunzo yanayotolewa bure chuoni hapo ili wasiachwe nyuma katika kazi zao.
.
Mshiriki akitolea ufafanuzi jambo.
Baadhi ya washiriki.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments