20 Percent : Narudi Kwenye Muziki Kuondoa Mziki wa Matusi Uliotawala | ZamotoHabari.


Baada ya kimya cha muda mrefu Mwanamuziki 20 Percent aliibukia na kutumbuiza katika tamasha la Chama cha Mapinduzi lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru siku ya Jumamosi

Baada ya kumaliza kutumbuiza amesema anafarijika kuona bado mashabiki wake wana upendo naye na bado anaishi mioyoni mwao kwani alipotumbuiza mashabiki wengi walimshangilia sana

Akihojiwa kutokana na mabadiliko ya muziki wa sasa akirejea atabadilika au ataendelea kufanya muziki wake wa zamani, 20 Percent ameahidi kurejea na kuleta muziki wa heshima na kukimbiza muziki wa matusi aliodai umetawala kwa sasa

Aidha, akihojiwa kuhusu kufanya muziki kuendana na soko la sasa, 20 Percent amesema “Mimi silengi soko, nalenga fikra za mlalahoi na mtu yeyote ambaye huzuni yake ipo na hamna mtu wa kuiongelea.”

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini