Daktari kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dkt William Mawala, amesema kuwa mtu anayepitisha gesi yenye harufu kali inaweza kuwa ni kiashiria cha tatizo mwilini ikiwemo matatizo kwenye mfumo wa chakula.
Akizungumza na SupaBreakfast ya East Africa Radio hii leo Agosti 27, 2020, Dkt Mawala amesema kuwa binadamu hutoa gesi mara 5 mpaka mara 15 kwa siku, ikiwa ni jambo la kawaida kwa mwili kufanya hivyo kutokana na kazi za mwili.
"Kupitisha gesi kwa wingi kwenye njia ya haja kubwa, inaweza kuwa ni ya kimyakimya na isiyo na harufu au ya sauti na inaweza kuwa ni mchakato wa kawaida au shida kwenye mfumo wa chakula, sababu inayosababisha ni ulaji wa vyakula vyenye nyuzi lishe nyingi kwani huchelewa kumeng'enywa, vyenye madini ya sulphur, mayai, nyama, zingine ni athari za madawa mbalimbali na kuwa na tatizo la kutokupata choo kwa muda mrefu", amesema Dkt Mawala
Amesisitiza watu kuacha kutafuna 'bigjii', kula harakaharaka na kuacha kunywa vinywaji vyenye gesi ili kuepukana na tatizo la tumbo kujaa gesi.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments