KOCHA mpya wa klabu ya Yanga, Zlatko Krmpotic, amewasili nchini leo Jumamosi, Agosti 29, 2020, asubuhi tayari kwa kuanza kutekeleza majukumu yake mapya ya kukinoa kikosi hicho cha Wanajangwani.
Zlatko ambaye ni raia wa Serbia amepewa kazi hiyo baada ya chaguo la kwanza la Yanga, Kocha Cedric Kaze, kushindwa kufika kwa wakati kutokana na matatizo ya kifamilia.
Pichani juu Zlatko akipokelewa na Msemaji wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments