MAJADILIANO KUBADILISHANA UZOEFU KUHUSU MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO YA KIJAMII, SHERIA ZAKE YAFANA | ZamotoHabari.


Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MAJADILIANO ya siku mbili yaliyolenga kubadilishana uzoefu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao kwa sasa na baadae yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa baada ya wadau wa mitandao ya kijamii kutoa maoni yao kwa kuangalia Sheria ya mtandao nchini.

Wakati wa majadiliano hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa kuhusisha makundi mbalimbali ya kijamii yakiwemo ya wanasheria, yameshirikisha pia wadau wengine wa nchini Nigeria waliotumia nafasi hiyo kutoa maoni , ushauri na mapendekezo kama njia mojawapo ya kuziomba Serikali za nchi hizo mbili kuangalia jinsi ya kuboresha sheria ya mtandao kwa siku za baadae.

Akizungumza kwa njia ya mtandao wakati akifunga majadiliano hayo akiwa nchini Nigeria Meneja Programu wa Shirika la Paradigm Initiative nchini humo Boys Adegoka amesema amefarijika kwa namna ambavyo kumekuwepo na ushirikiano mkubwa wa kuchambua sera na sheria ya mitandao ya kijamii iliyopo nchi za Tanzania na Nigeria.

Kuhusu majadiliano hayo Boys Adegoka amesema hiyo ni hatua ya pili ya mchakato waliouanzisha kuelekea kuulinda usalama wa watumiaji wa huduma za mtandao.

"Tutakuwa tukifanya kazi na wadau mbalimbali katika mchakato huu. Kwa ujumla mazingira ya Sera ya Dijitali ya Tanzania pamoja na mafanikio bado changamoto nyingi. Hivyo basi kuna haja ya kuzipunguza ama kuziondoa kabisa hizo changamoto kwa siku za baadae kwa kufuata utaratibu sahihi,"amesema.

Hata hivyo amefafanua msingi wa sheria iliyopendekezwa umejengwa juu ya juhudi kama hizo zinazoendelea katika nchi za Nigeria, Kameruni na Togo. "Kwa sasa, tutaendelea kuyashirikisha ama kushirikiana na mashirika mbalimbali ambayo yanafanya kazi kubwa katika kujenga umoja na ushirikiano madhubuti ili kuelekea kuyafikia malengo yaliyowekwa.

" Pamoja na hayo, tutakuwa tukiihusisha Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Tanzania na Wizara ya Mawasiliano katika kujadili pendekezo hili kabla ya kuanza tena kwa shughuli za Bunge baada ya uchaguzi mkuu,"amesema Meneja huyo wa Programu kutoka Shirika hilo la Paradigm Initiative nchini Nigeria.

Awali alipokuwa akizungumzia majadiliano hayo Mratibu wa majadiliano hayo nchini Tanzania Peter Mmbando amesema ni wakati mwakafa wa kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na nchi nyingine za Afrika ili kuona nini cha kujifunza kuendana na wakati kwa mahitaji ya sasa na baadae.
 Picha ambazo zinaonesha matukio tofauti wakati wadau wa masuala ya mitandao ya kijamii walipokutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kubadilisha uzoefu ikiwa pamoja na kuangalia sheria ya mtandao iliyopo.

 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini