Baba mzazi wa lionel Messi amekanusha taarifa iliyonukuliwa na moja ya chombo za habari nchini Argentina kuwa mwanae ameshafanya maamuzi yakujiunga na klabu ya Manchester City ya England.
Lionel Messi anatajwa kutokuwa na furaha ndani ya kikosi cha FC Barcelona kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo ya kikosi hicho
Siku ya jumanne usiku mchezaji huyo bora wa Dunia mara sita alipeleka maombi yakuomba aondoke katika klabu ya FC Barcelona, klabu ambayo alijiunnga nayo akiwa na umri wa miaka 12.
Inaaminika kuwa mktaba wa Messi na klabu ya Barcelona kuna kipengele ambacho kilikuwa kinamruhusu mchezaji huyu kuondoka akiwa mchezaji huru baada ya msimu wa 2019-20 kumalizika. Lakini pia kipengele hicho cha kumruhusu Messi kuondoka akiwa mchezaji huru kinaonyesha ukomo wake ilikuwa juni 10.
Kutokana na msimu kumalizika mwezi August kutokana mlipuko wa virusi vya Corona Messi ameuambia uongozi wa klabu hiyo kuwa bado ana nafasi ya kukitumia kipengele hicho kuvunja mkataba na Barcelona.
Manchester city inatajwa kuwa ndio klabu iliyo kwenye nafasi nzuri ya kumsajili nahodha huyu wa Argentina mwenye umri wa miaka 33, kutokana na uwepo wa Kocha Pep Guardiola ambaye aliwahi kufanya kazi na Messi katika klabu ya Barcelona na utajiri mkubwa wa wamiliki wa timu hiyo.
Gazeti moja la nchini Argentina La Nacion jana Jumatano lilichapisha nukuu ambazo zilitoka kwenye moja ya sauti ambayo inaaminika yalikuwa ni mazungumzo ya Messi na mke wake Antonela Roccuzzo wakizungumza juu ya hatima ya mchezaji huyo, nukuu hizo zilithibitisha kuwa mchezaji huyo amefikia makuballia na mkewe kuondoka Barcelona lakini pia akisema anaelekea kujiunga na Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City.
Jorge Messi baba mzazi na wakala wa mchezaji Lionel Messi, amekanusha taarifa za mwanae kujiunga na Manchester City
Lakini baba mzazi wa mchezaji huyu Jorge Messi ambaye pia ni wakala wake amekanusha kuwa taarifa hiyo ni batili.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram wa baba mzazi wa Messi aliweka picha ya taarifa hiyo iliyotolewa na gazeti la La Nacion na kuandika ‘taarifa hii ni batili’.
Lakini pia La Nacion nao wakajibu kuwa hawakunukuu taarifa hiyo kutoka kwenye sauti yoyote lakini walipata kutoka kwa chanzo cha karibu na mchezaji huyo.
Zinatajwa sababu nyingi za zinazomfanya Messi kufikia uamuzi wa kutaka kuondoka Barcelona, kutoridhishwa na utendaji wa uongozi wa klabu hiyo chini ya Rais Josep Maria Bartomeu ni moja ya sababu lakini pia kipigo cha mabao 8-2 dhidi ya Bayern Munich pia inatajwa ni moja ya sababu.
Timu nyingine zinazotajwa kumuwania Lionel Messi ni Juventus ya Italia, Manchester United ya England na PSG ya nchini Ufaransa.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments