TAMASHA LA IRINGA ALL STARS KUFANYIKA CLUB V.I.P | ZamotoHabari

Na Denis Mlowe, Iringa
TAMASHA kubwa lijakulikana kwa jina la Iringa  All Stars linatarajiwa kufanyika kesho kwenye ukumbi wa Klabu VIP na kuwakutanisha mastaa mbalimbali wanaoishi mkoani Iringa.

Tamasha hilo  linaloandaliwa na mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Finest Ramadhan Shemhilu lina lengo la kutengeneza kipato kwa wasanii wanaoishi mkoani hapa kujikomboa kiuchumi.

Akizungumza na mwanahabari hizi, Shemhilu alisema kuwa licha ya kuwaongezea kipato wasanii lina lengo pia kuwakutanisha mashabiki zao ambao wamekuwa wakiwasikia katika vyombo mbalimbali vya habari mkoani hapa.

Alisema kuwa tamasha hilo ni la kujivunia cha kwa wasanii mbalimbali ambapo kutakuwa na tasnia mbalimbali za burudani ikiwemo sanaa ya uchekeshaji.

"Licha bongo fleva kutakuwa na burudani mbalimbali kama Maonyesho ya mavazi na live band kutoka bendi za  Iringa." Alisema

Aliongeza kuwa tamasha hilo litakuwa mahususi kwa wasanii na vijana mbalimbali kuonyesha vipaji vyao ambao Kuna wadau mbalimbali wameahidi kuwasaidia vijana hao.

Alisema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kikubwa ni watu kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji mbalimbali ikiwemo wasanii wa bongo movie mkoani hapa kuonyesha kazi zao.

Aidha alisema kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mgombea ubunge Iringa Mjini kwa tiketi ya CCM Jesca Msambatavangu na litaanza kuanzia saa moja usiku.

Mratibu wa tamasha la Iringa All Stars mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Finest Ramadhan Shemhilu.

Baadhi ya wasanii wakiwa kwenye mazoezi ya tamasha hilo.
(Picha zote na Denis Mlowe)


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini