Tweet ya taarifa ya kifo iliyotolewa kwenye ukurasa wa aliyekuwa staa wa filamu nchini Chadwick Boseman, imeweka rekodi mpya kwa kuongoza kwa watu 'likes' na ku-retweet mara nyingi zaidi tangu mtandao wa Twitter uanzishwe.
Tweet hiyo imepata likes Milioni 6.3 na retweet Milioni 2.1, hii inaonyesha jinsi gani dunia imesikitishwa na kuguswa kwa taarifa za kifo chake kilichotokea siku ya kuamkia August 29, 2020 nyumbani kwake Los Angeles mbele ya mkewe na familia yake.
Chanzo cha kifo chake kinaelezwa kuwa kimesababishwa na Ugonjwa wa Kansa ya Utumbo ambayo amepambana nayo kuanzia mwaka 2016 na mpaka umauti unamkuta alikuwa na miaka 43.
Staa huyo amepata umaarufu mkubwa kupitia filamu ya Black Panther au Wakanda Forever ambayo ilitoka mwaka 2018
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments