Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Wachangia Milioni 30 Ujenzi wa Msikiti Chamwino | ZamotoHabari.


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo akimkabidhi Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Charles Mbuge mchango wa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa ajili ya ujenzi wa msikiti wa Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma unaojengwa na SUMA JKT ambaye ni mkandarasi wa mradi huo.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Charles Mbuge akizungumza wakati wa hafla ya kupokea mchango wa Wakuu Vyombo vya Ulinzi na Usalama waliochangia milioni 30 na Wakuu wa Mikoa ambao wamechangia shilingi Milioni 26 katika ujenzi wa msikiti wa Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma 




Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo akisalimiana na wakuu wa mikoa katika hafla ya kukabidhi mchango kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti wa Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.


PIX1.Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo akizungumza
wakati wa hafla ya kukabidhi mchango wa shilingi milioni 30 zilizotolewa na Wakuu wa
Vyombo vya Ulinzi na usalama kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti wa Wilaya ya Chamwino
jijini Dodoma. 


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evaristi Ndikilo akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa wakati wa hafla ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Wilaya Chamwino jijini Dodoma.


Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Charles Mbuge akikabidhiwa mchango wa shilingi milioni 26 na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evaristi Ndikilo kwa niaba ya wakuu wa mikoa wakati wa hafla ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Wilaya Chamwino jijini Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Charles Mbuge akikabidhi mchango uliochangwa na Kanisa la AIC Simiyu, na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa hafla ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Wilaya Chamwino jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakuu wa Mikoa walishiriki katika hafla hiyo wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo kabla hajakabidhimchango wa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuwezesha ujenzi wa Msikiti waWilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.


Shehe wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Bw. Suleiman Matitu akitoa neno la shukrani kwa Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama na Wakuu wa Mikoa waliochangia katika ujenzi wa msikiti wa Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma

………………………………………………………………….


Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wamekabidhi Shilingi milioni 30 ujenzi wa msikiti wa kisasa wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Akikabidhi mchango huo leo Agosti 27, 2020 kwa niaba ya wakuu wengine wa vyombo hivyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo amesema kuwa wameguswa na azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwawezesha wananchi katika masuala mbalimbali ikiwemo ya imani .

“Naamini kuwa michango zaidi itaendelea kutolewa ili azma ya kujenga msikiti huu ikamilike kwa wakati”, Alisisitiza Jenerali Mabeyo

Hafla ya Kukabidhi fedha hizo imefanyika pembezoni mwa msikiti wa zamani unapojengwa msikiti huo mpya ambapo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Venance Mabeyo amekabidhi fedha hizo kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali, Charles Mbuge, ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Suma JKT, inayotekeleza mradi huo.

Naye Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Charles Mbuge amesema kuwa kiasi cha Shilingi milioni 142 zimeshachangwa na wadau mbalimbali ili kuwezesha ujenzi wa msikiti huo.

Alipongeza jitihada za kuwafanya watanzania kushikamana bila kujali imani zao kutokana na ushirikiano ulioneshwa na wadau mbalimbali katika kuchangia ujenzi wa msikiti huo.

Kwa upande wa Wakuu wa Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara,nao pia wamekabidhi shilingi milioni 26 kwaajili ya Ujenzi huo.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa Mikoa hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evaristi Ndikilo amesema kuwa wanaunga mkono juhudi za ujenzi wa msikiti huo zilizoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Aidha, Pamoja na Fedha hizo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka,amekabidhi shilingi milioni mbili zilizochangwa na kanisa la AICC la mkoani humo.

Kwa upande wake, Sheikh mkuu wa Wilaya ya Chamwino Suleiman Matitu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuchangia ujenzi wa msikiti huo na kuhamasisha wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia.

Aidha, Shehe Matitu aliwashukuru Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Wakuu wa mikoa kwa kuchangia ujenzi wa msikiti huo.

Azma ya kujenga msikiti mpya wa Wilaya ya Chamwino ilianzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni wakati wa ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa Katoliki la Mt. Immaculata Chamwino ambapo alizindua kanisa hilo baada ya kuchangia ujenzi wake na ukarabati.

Katika kuendeleza azma hiyo alianzisha harambee ya ujenzi wa msikiti huo ambapo hadi sasa kiasi cha Shilingi Milioni 142 zimeshapatikana.

Ujenzi wa Msikiti huo unatekelezwa na Mkandarasi ambaye ni SUMA JKT na tayari vifaa na malighafi mbambali zimeanza kufikishwa katika eneo la ujenzi ili kazi ya ujenzi iweze kuanza mara moja.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini