Wema Sepetu : Sina ‘Tatuu’ ya Mwanaume Mwilini Mwangu | ZamotoHabari.


STAA mwenye jina kubwa Bongo, Wema Sepetu amefunguka kuwa kamwe hawezi kuchora tatuu ya jina la mwanaume mwingine yeyote kwenye mwili wake zaidi ya baba yake mzazi.

Akizungumza na AMANI, Wema alisema hata mwanaume afanye maajabu gani katika maisha yake, hawezi kumchora mwanaune yoyote kwenye mwili wake zaidi wazazi wake.

“Yaani mwanaume ambaye nimempa nafasi ya kumchora kwenye mwili wangu ni baba yangu peke yake na si mtu mwingine maana sijaona maajabu aliyofanya mwanaume kwangu mpaka nimchore. Hata akiyafanya bado hana nafasi ya kumchora kwenye mwili wangu maana hawaaminiki” alisema Wema.

Stori: Imelda Mtema



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini