Zlatan ni mali ya Ac Milan | ZamotoHabari.


Mshambuliaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Sweden ,Zlatan Ibrahimovich ameongeza mkataba wa mwaka moja zaidi ili kundelea kubakia katika kikosi cha Ac Milan.



Zlatan moja ya washambuliaji  bora kuwahi kutokea duniani, ataendelea kusalia Jijini Milan na hii inatokana na kufaya vizuri katika msimu uliomalizika akiwa na wababe hao wa Italia kwa miaka ya nyuma.

Bodi ya AC Milan imethibitisha  kufanya naye mazungumzo ya kumpa mwaka moja zaidi na nyota huyo amethibitisha kuwa ataendelea kuipigania klabu hiyo.

JE ATAISAIDIA MILAN?

Anauzoefu mkubwa akiwa amecheza katika vilabu mbalimbali mfano Ajax alikoanza safari yake,Juventus,Inter Milan,Barcelona,PSG ,na Manchester United hiyo inatosha kuonyesha anauwezo mkubwa na mikiki mikiki ya ligi kubwa pia.

Serie A kwake ni kama nyumbani, na katika michezo 20 aliyocheza nusu msimu uliomalizika,alifunga mabao 11 na kuipa uhai Timu hiyo ambayo ilionekana kuyumba mwanzini mwa msimu.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini