MAWASILIANO NI JAMBO MUHIMU SANA KWA JAMII KWASABABU HULETA MAENDELEO NA KUFANYA UCHUMI UKUE | ZamotoHabari.

MGOMBEA ubunge jimbo la Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Hamisi Ulega amesema mawasiliano ni jambo muhimu sana kwa jamii Kwasababu huleta maendeleo na kufanya uchumi ukuwe.  

Ulega  ameyasema hayo  katika Kata ya magawa wilayani mkuranga mkoani pwani wakati wa kampeni ambapo ametembelea ujenzi wa mnara wa simu unaoendelea katika Kata hiyo na kusema ujenzi huo utarahisisha mawasiliano yawatu na biashara.  

Aidha Ulega amesema mpaka sasa minara mitano inajengwa katika wilaya ya mkuranga ambapo ukiacha kata ya magawa pia kuna bupu na mbezi hivyo ameahidi wanachi kuwa changamoto ya mawasiliano mkuranga inaenda kuwa historia.

Pia mgombea ubunge huyo amesema ukiacha ujenzi wa  mnara katika Kata ya magawa ameshatoa ushirikiano Sana katika maendeleo ikiwemo barabara,afya na elimu nakuomba wananchi kukipa tena miaka mitano chama cha mapinduzi ili wakafanye maajabu katika maendeleo. 

Hata hivyo ulega ameongeza kuwa endapo wananchi wa magawa watamchagua  basi ataunga mkono ujenzi wazahanati ya makumbea kwa kutoa bati 150  ili kuboresha huduma za afya na kwa upande wa umeme amesema atamsisitiza mkandarasi ili mradi unaondelea katika kata hiyo uwezekukamilika kwa wakati. 

Hata hivyo  ulega hakuishia  magawa bali aliendelea na kampeni katika Kata ya msonga na kuwataka wananchi wa hapo kuendelea kukiunga mkono chama cha mapinduzi kwa kukipa kura nyingi na kuwaahidi , kuwa kupitia ilani ya chama watatuliwa changamoto zao za afya, elimu pamoja na miundo mbinu. 

Aidha Ulega ameeleza kuwa msonga imekuwa kama kisiwa kutokana na changamoto ya barabara,ambazo nyingi hazipitiki  lakini amewatoa hofu wananchi kuwa barabara zote zitafunguka na uchumi utakuwa miongoni mwao.

Kwa upande wake Juma Othmani Abeid ambaye ni mgombea udiwani kata ya magawa amewambia wananchi kwamba mpaka ifikapo mwezi October mnara huo utakuwa umekamilika na vijiji vyote vitano vya kata hiyo vitaondokana na changamoto ya mawasiliano.
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega (kulia) akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi leo katika Kata ya Magawa wilayani mkuranga mkoa wa Pwani.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini