Na Woinde Shizza ,ARUSHA
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amezitaka Taasisi na Makampuni mbalimbali yanayojishughulisha na shughuli za ulinzi Wilayani humo kuhakikisha yanaajiri walinzi waliopata mafunzo ya jeshi la akiba ili kuleta tija kwenye kuimarisha ulinzi na usalama Wilayani humo.
Aliyasema hayo juzi wakati akifunga rasmi mafunzo ya jeshi la akiba kundi 6/2020 yaliyoanza 24 februari 2020 katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru,zoezi lililofanyika katika viwanja vya Relini, Kata ya Usa River. Mkuu huyo wa Wilaya amezitaka Ambapo alisisitiza ni muhimu taasisi na Makampuni mbalimbali yanayojishughulisha na shughuli za ulinzi Wilayani Arumeru kuhakikisha yanaajiri walinzi waliopata mafunzo ya jeshi la akiba .
Aidha, Muro alipongeza timu ya jeshi la akiba Wilaya ya Arumeru ikiongozwa na Kapteni. Issack Kimaryo kwa kuratibu mafunzo hayo kwani wahitimu wote 170 ambao wanaume ni 118 na wanawake ni 52 wameonyesha umahiri na uelewa wa hali ya juu uwanjani hapo hivyo kupelekea makampuni ya ulinzi ikiwemo Suma JKT guard, Cachson Risk management, SGA security, GB security, ADF security kuhitaji kuwaajiri Askari wote 170 waliohitimu.
“fursa ya ajira ni kubwa kwani mliohitimu hamtoshi uhitaji wa Makampuni haya,natoa wito kwa vijana kujitokeza kushiriki mafunzo yanapotangazwa “amesisitiza Muro
Akihitimisha, Muro alitoa wito kwa wahitimu hao kutumia mafunzo waliyopewa kudumisha amani na ulinzi wa raia na mali zao sambamba na kuwa na nidhamu."Nidhamu ni dhana na silaha namba moja ya askari katika swala zima la ulinzi " amesisitiza Muro.
Mshauri wa jeshi la akiba wilaya ya Arumeru, Kapteni. Issack Kimaryo akisoma taarifa alisema kundi la 6/2020 lilianza mafunzo tarehe 24/02/2020 likiwa na wanafunzi 184 wakiwemo wanaume 124 na wanawake 60 lakini hadi kufikia tarehe ya kuhitimu wamebaki 170 ambapo 14 wameshindwa kuhitimu mafunzo kutokana na sababu mbalimbali.
Aidha, Kapteni.Kimaryo alisema mafunzo hayo ya awali ya ulinzi na usalama wa umma yamechukua majuma 18 ambapo askari walifundishwa masomo ya silaa, kwata, huduma ya kwanza, usomaji ramani, mbinu za kivita ,ujanja porini ,utimamu wa mwili na sheria za jeshi la akiba hivyo askari hao wamekidhi vigezo vyote vya jeshi la akiba na wako tayari kulitumikia taifa katika ulinzi wa umma kwa maendeleo ya taifa na majuku mengine watakayo pangiwa katika kusaidia taasisi za umma .
Wahitimu wa mafunzo hayo Deborah Dorothea wameishikuru Serikali kwa kuanzisha mafunzo hayo ambayo yamezaa matunda kwa kufungua fursa ya ajira kwa vijana pia waliweza kujifunza ukakamavu na elimu juu ya afya .
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments