Chama cha Act-Wazalendo kimehitimisha kampeni zake za Urais visiwani Zanzibar, ambapo mgombea urais kupitia chama hicho, Maalim Seif Hamad, ametoa tathimini juu ya kampeni zake alizozifanya visiwani humo.
Kushoto ni mgombea urais kupitia chama cha Act-Wazalendo Maalim Seif Hamad na kushoto ni umati wa wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wake wa kufunga kampeni Unguja.
Akizungumza leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja visiwani humo Maalim amewahimiza wazanzabari kujitokeza siku ya kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi wanaowahitaji.
"Tumefanya kampeni na kwa tathimini yangu ni nzuri tuliwaeleza dhamira zetu,ahadi zetu na nini mtegemee kutoka kwetu ikiwa nitakuwa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi" amesema Maalim Seif
Aidha Maalim aliendelea kugusia mambo makubwa ambayo watayatekeleza endapo watapewa idhini na wananchi kuiongoza Zanzibar.
"Mambo mengi tumesema kubwa kuboresha maisha kuhakikisha kila mzanzibari anapata ajira ,kuhakikisha vijana wetu wanapata elimu nzuri bila ya gharama mzazi" amesema Maalim Seif
Leo chama cha ACT Wazalendo kimefunga kampeni zake visiwani humo zikiwa zimebaki siku chache hadi kufikia tarehe 28/10 ambapo wananchi wataenda kupiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi wanaowahitaji.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments