Bodi ya Korosho yakanusha salfa kukausha maua ya korosho | ZamotoHabari.

Na ANNE ROBI Mtwara

BODI ya Korosho nchini (CBT) imesema taarifa zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kuwa mikorosho nchini inakauka kwa sababu ya matumizi ya salfa sio za kweli huku ikiwataka wananchi na wadau wengine wa zao hilo kuzipuuza.

Kaimu Mkurungezi Mkuu wa Bodi hiyo Francis Alfredy amewaambia waandishi wa habari kwamba hakuna mikorosho iliyokauka katika mikoa yote 17 inayolima kutokana na matumizi ya salfa.

“Napende kukanusha kuwa taarifa hizo sio za kweli, hakuna mikorosho iliyokauka katika mikoa yote 17 inayolima korosho kutokana ka matumiza ya salfa,” amesema.

Francis ameeleza kwamba hali ya baridi iliyotokana na kushuka kwa joto chini ya sentigrade 20 hadi kufikia nyuzi joto sentigrade 17 kuanzia mnamo mwezi Julai hadi Agosti mwaka huu ndio uliopelekea kukauka kwa maua ya mikorosho.

“Katika msimu wa 2020/2021 kilichotokea ni kwamba mwishoni mwa mwezi Julai maua ya mikorosho yalianza kukauka hali hiyo iliendelea hadi mwezi Agosti. Hali hii hutokea pale joto linapopanda kuzidi sentigradi 30 au kuwa chini ya sentigradi 20. Maua ya mikorosho yanaweza kukauka,” amesema.

Amesema maua ya mikorosho hustawi na kutoa mazao katika kiwango cha joto kati ya sentigradi 20 had 30 huku akiongeza kwamba katika katika kipindi cha mwezi Julai hadi Agosti mwaka huu kulikuwa na viwango vya joto chini ya sentigradi 20 katika ukanda wa Pwani pamoja na mikoa ya Lindi, Mtwara, Lindi na baadhi ya maeneo ya Ruvuma.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) ilitoa taarifa mwezi Juni juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwa ni pamoja na kushuka kwa viwango vya joto katika ukanda wa Pwani. Kwa mujibu wa CBT, hali hiyo ya baridi (joto chini ya sentigradi 20) ilichangia kukauka kwa maua.

“Hii inajiridhisha kutokana na ushahidi kuwa maua yamekauka kwenye maeneo yote ya ukanda wa Pwani, ambayo yalipuliziwa salfa na ambayo hayakupuliziwa salfa,” amesema.

Hata hivyo, Francis amesema halia ya ustawi wa maua hayo yameaza kurudi kutokana na kiwango cha joto kuanza kupanda. “Mashahada ya ambayo maua yake yalikuwa yamekauka yameanza kutoa maua mapya kuanzia mwezi Septemba ambapo kiwango cha joto kilikuwa kimeanza kupanda,” amesema.

Francis amewataka wakulima kuendelea kuhudumia mashamba yao pamoja na kutumia viuatilifu kwa kuzingatia ushauri wa kitaalam ili maua hayo yaweze kuzaa korosho.

Akitoa ufafanuzi
kuhusu matumizi ya salfa katika zao la korosho, Francis amesema upulizaji wa salfa huanza mwezi wa Mei mpaka Agosti na huambatana na matumizi sahihi ya viuatilifu vya maji.

Amesema katika msimu wa 2020/2021 vyama vikuu vya ushirika viliwawezesha wakulima kupata viuatilifu hivyo kwa wakati na kuvitumia kwa usahihi. Amesema kuwa katika msimu wa 2020/2021, kunna ongezeko la uzalishaji wa korosho ukilinganisha na msimu uliopita.

“Katika msimu wa 2020/2021 mategemeo ni kupata tani 278,000 ilikinganishwa na mwaka juzi 2018/2019 ambapo ilikuwa ni  tani 225,000 na mwaka jana 2019/2020 tulipata tani 232,000,” amesema na kuongeza kuwa ongezeko la uzalishaji katika miaka mitatu mfululizo linachangiwa na matumizi sahihi ya viuatilifu, vyeny ubora ambavyo husambazwa kwa wakati.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini