Carlos Tusguets ateuliwa rais wa muda wa Barcelona | ZamotoHabari.



Mfanyabiashara na mchumi Carlos Tusguets, amechaguliwa kuwa Rais wa muda wa klabu ya soka ya Barcelona, kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Rais wa klabu hiyo Joseph Maria Bartomeu.

 

 Tusguets atalazimika kuongoza kwa miezi kadhaa hadi uchaguzi mkuu wa klabu ufanyike mwezi Machi 2021.


Tusguets raia wa Hispania ni mtu anayeheshimika sana nchini humo, kutokana na uwekezaji wake na kuongoza taasisi mbalimbali za fedha nchini humo na bara zima la Ulaya, pamoja na kufanya kazi na zaidi ya makampuni makubwa 56 duniani.


Carlos Tusguets kwa sasa ana umri wa miaka 80, amekuwa mkosoaji hadharani kwa uongozi wa Joseph Maria Bartomeu, kufuatia mwenendo wa timu katika utawala wake hadi kufikia kujiuzulu.


Bartomeu aliingia madaraka mwaka 2014 baada ya mtangulizi wake kwenye nafasi ya urais Sandro Rosell kujiuzulu. Mwaka uliofuata (2015) aliipa Barcelona mafanikio makubwa ya kushinda mataji matatu ambayo ni La Liga, Kombe la mfalme na Kombe la klabu bingwa Ulaya.


Kujiuzulu kwa Bartomeu katika nafasi ya urais, zinatajwa sababu mbalimbali ikiwemo ya kuyumba kiuchumi, kushindwa kusimamia vyema matumuzi ya mitandao ya kijamii ya klabu, lakini kubwa kuliko yote ni matokeo mabaya ya kufungwa 8-2 na Bayern Munich katika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa msimu wa 2019-2020.



 

Haijulikani kama Tusguets ataomba ridhaa ya kuingoza klabu katika uchaguzi mkuu, japo wanachama wengi wameonesha imani naye kwa sababu ya uwezo wake wa kuongoza taasisi kubwa za fedha wakiamini atawaletea mafanikio akitumia ufahamu wake wa mambo ya fedha kurudisha uchumi wa klabu kwenye sehemu yake baada ya kuporomoka.


 



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini