Mkuu wa Wilaya ya Magu,Salum Kalli akizungumza na walimu wa shule za sekondari na msingi zilizo kwenye Tarafa ya Itumbili jana kuhusu suala la mimba na uchaguzi mkuu.Picha na Baltazar Mashaka
Mkuu wa Wilaya ya Magu,Salum Kalli akisistiza jambo wakati akizungumza na walimu wa shule za sekondari na msingi zilizo kwenye Tarafa ya Itumbili jana kuhusu suala la mimba na uchaguzi mkuu.Picha na Baltazar Mashaka
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Magu, Mrakibu wa Polisi Mahamoud Banga jana akizungumza na walimu wa shule za sekondari na msingi za Taraf ya Itumbili (hawapo pichani) kwenye mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Salum Kalli, wa pili kutoka kulia walioketi.Mkutano huo ulifanyika Magu sekondari.
Walimu wa shule za sekondari na msingi za Tarafa ya Itumbili wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum Kalli (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa walimu uliofanyika kwenye ukumbi wa shue ya Magu sekondari jana.
…………………………………………………………………….
NA BALTAZAR MASHAKA,Magu
Alisema yeye pia kama mzazi hafurahishwi na vitendo hivyo viovu wanavyofanyiwa watoto na walimu wao hasa wa kiume na kuonya watoto hao ni viongozi watarajiwa wa taifa hii hawapaswi kufanyiwa hayo.
Kalli alisema baadhi ya walimu wilayani Magu kufanya mapenzi na watoto wadogo wa shule za msingi na sekondari vitendo hivyo vinaumiza mno na kwamba katika shule ya msingi Irungu mwalimu mwenye umri zaidi ya 50, kwa miaka saba amekuwa akiwaingilia watoto wa kiume kinyume cha maumbile.
Alidai mwalimu huyo wa shule ya msingi Ilungu, Tarafa ya Itumbili (Mambosasa) amewaharibu watoto wa kiume kwa kuwaingilia kinyume cha maumbile na kawapa ujauzito wasichana watatu ambapo mwalimu mmoja wa Tarafa ya Ndagalu (Abdul 48) yeye kamweka kinyumba huko wilayani Kwimba, mwanafunzi wa darasa la nne baada ya kumpa ujauzito.
“Kuna mwalimu shule ya Msingi Irungu ana umri wa miaka zaidi ya 53 (akamtaja) huyo namtafuta amekuwa akiwaingilia watoto wa kiume kwa miaka 7,kawapa mimba watoto watatu,wawili wa darasa la V amewasaidia kutoa, ila mmoja wa dasara la VII imeshindikana,” alisema Kalli.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kati ya wanafunzi hao mmoja ameathirika na kamuanzishia matumizi ya dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV’S) na kibaya zaidi wakati akifanya nao ngono alikuwa akiwalaza kitanda kimoja na kuwalipa sh. 10,000 kwa kuigawanya kulingana na jinsi kila mmoja alivyomhudumia.
“Huyo mwalimu wa Irungu, kwa miaka 7 amewaharibu watoto na kila akitafutwa hata akiwapo shuleni wenzake wanamficha sasa naagiza atafutwe popote alipo akamatwe.Mwingine wa Tarafa ya Ndagalu mwenye miaka 48 kampa mimba na kumweka kinyumba mwanafunzi wa darasa la nne, kakimbia, naye namtafuta,”alisema Kalli na kumwagiza Mkuu wa Polisi wilayani humo kuwasaka na kuwakamata au wajisalimishe wenyewe.
Alisema kuwa vitendo hivyo vya ovyo vinavyofanywa na walimu wilayani Magu vinaichafua wilaya hiyo pamoja na jina la Rais John Magufuli ambaye pia ni mwalimu mwenzao na kuwaagiza wakuu wa shule kusimamia nidhamu na uadilifu wa walimu kwani mwalimu ni mtu mwenye akilina msafi lakini kwa Magu ni kinyume chake.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya hiyo (DAS) Manref Nyoni alisema serikali itazidisha ukali kwa walimu wanaokiuka maadili na kufanya mapenzi na wanafunzi na hata watakaofikishwa mahakamani wakashinda kesi kwa sababu ya ushahidi kutojitosheleza watafukuzwa kwa mujibu wa sheria.
Naye Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Magu, Mwita Gisiri, alisema mwaka 2018-2020 walimu sita walifukuzwa kazi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na wanafunzi na kuwataka walimu kutokubali kupoteza kazi kwa makosa ya uzembe na tamaa za kimwili, ambao hawajaoa waoe ili wasiidhalilishe taaluma ya ualimu.
Aidha Mkuu wa Polisi Magu, Mahamoud Banga alisema walimu wa kike wamepoteza mwelekeo wa malezi,wameingia kwenye msemo wa mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzio na ili kuwanusuru wanafunzi na mimba za utotoni walimu wakuu waweke mkakati shuleni wa kuchunguza tabia za walimu wanaotongoza wanafunzi ili kukwepa gharama za mtaani.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments