DK.JOHN MAGUFULI APIGA KURA, ATOA UJUMBE WA AMANI KWA WATANZANIA | ZamotoHabari.

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Chamwino

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Magufuli ametimiza wajibu wake wa kikatiba wa kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo Oktoba 28 mwaka huu huku akitumia nafasi hiyo kusisitiza umuhimu wa kutunza amaní kabla na baada ya uchaguzi.

Dk.Magufuli amepiga kura katika kituo cha kupiga kura Idara ya Maji Chamwino-Ikulu ambapo alifika kituoni hapo saa tatu asubuhi akiwa ameongozana na mkewe mama Janeth Magufuli.

Baada ya kufika katika hicho Dk.Magufuli na Mama Janeth walipanga foleni kama ambavyo wamepanga wapiga kura wengine na alifuata mstari hadi jina lake lilipfika, hivyo akaingia ndani kupiga kura yake.Jina la Mama Janeth Magufuli lilikuwa la kwanza kuitwa na kuingia kupiga kura.

Alipomaliza kupiga kura,Dk.Magufuli ametumia nafasi hiyo kueleza amefurahishwa na utaratibu mzima wa upigaji kura kituoni hapo huku akisisitiza umuhimu wa kudumisha amani kabla na baada ya uchaguzi mkuu.

“Nimeshapiga kura yangu na kidole change hiki hapa(akaoesha) , napongeza utaratib mzuri uliopo hapa kituoni, wananchi wengi wamejitokeza kupiga kura na niendelee kuwasisisitiza wale ambao bado hawajapiga waende wakatimize wajibu wao kikatiba,”amesema Dk.Magufuli.

Amewasisitiza wananchi wote nchini kuhakikisha wanendelea kuwa watulivu na kuendelea kulinda na kuitunza amani yetu kala na baada ya uchaguzi mkuu kwani kuna maisha baada ya uchaguzi.”

Kwa upande wake ,Msimamizi wa uchaguzi katika kituo hicho Othman Masasi amesema wananchi wengi wamejitokeza kupiga kura huku akitumia nafasi hiyo pia kuelezea kwamba Dk.Magufuli na mkewe Mama Janeth wamepiga kura katika kituo hicho.

“Uchaguzi unaendelea vizuri, watu wengi wamejitokeza na wanafuata utaratibu ambao umewekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), changamoto sio nyingi sana kwani inaonesha wananchi wengi wamekuwa na uelewa kuhusu kupiga kura,”amesema Masasi.

 


  

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakipiga kura ya Urais na Mbunge katika Kituo cha Kupigia Kura cha Idara ya Maji kilichopo katika Kijiji cha Chamwino Ikulu mkoani Dodoma leo tarehe 28 Oktoba 2020.

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwasili katika Kituo cha Kupigia Kura cha Idara ya Maji Chamwino Ikulu kwa ajili ya kupiga Kura leo tarehe 28 Oktoba 2020.

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa wamepanga mstari pamoja na Wapiga kura wengine katika Kituo cha Kupigia Kura cha Idara ya Maji kilichopo katika Kijiji cha Chamwino Ikulu mkoani Dodoma leo tarehe 28 Oktoba 2020.

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakifanya uhakiki kabla ya kupiga Kura katika Kituo cha Kupigia Kura cha Idara ya Maji Chamwino kwa ajili ya kupiga Kura leo tarehe 28 Oktoba 2020.

 

 



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini