DR. TULIA AFICHUA SIRI YA CCM KULICHUKUA JIMBO LA MBEYA MJINI | ZamotoHabari.

 


 

*************************************

Ni headline nyingine tena kutokea Jimbo la Mbeya Mjini ambapo mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia CCM Dr. Tulia Ackson leo October 8, 2020 alikuwa akiendela na kampeni zake katika kata ya Itagano ambapo amewaeleza Wananchi ni kwanini aiomba nafasi ya kuwatumikia katika nafasi hiyo.

Dr. Tulia amesema>>>”Wana-Itagano leo nitawaeleza ni kwanini nasema mpeni kura zote Tulia ambaye ni Mbozyo au dawa ya wana-Mbeya, kama mtu hatujawahi kumuona hapa kwetu katika kipindi chote akitusaidia wala hajafanya jambo lolote alafu anakuja leo kuomba kura huyo tunasukuma nje”- Dr. Tulia Ackson

“Sasa tukianza na Shule ya msingi Itagano, unataka kusikia mimi Tulia nimeshafanya nini hapo? Tumeshaleta mifuko 100 ya Cement baada ya kuletewa kilio cha changamoto wa uhaba wa miundombinu katika shule hiyo na tukafanya mambo haraka”- Dr. Tulia Ackson

“Hapa mmenieleza pia kuhusu changamoto ya Shule ya Sekondari Itagano ambayo imeanza kujengwa kitambo lakini hadi leo haijakamilika na watoto wetu hadi wavuke milima na mabonde ndio waende Sekondari sasa kwa mifano hii dawa ya changamoto hizo imepatikana na wajibu wenu ni mmoja tu wa kukiamini Chama Cha Mapinduzi ili tuweze kuzitatua kwa haraka”- Dr. Tulia Ackson

“Sisi wasafwa tuna neno letu tunaliita CONNECTIO, sasa nitawaeleza ni kwanini ni muhimu kumchagua Tulia aende Bungeni na Magufuli aende Ikulu kwasababu tunayo mawasiliano ambayo linapotokea jambo tunawasiliana na kwa haraka sana linatatuliwa. Sasa mnafikiri mkimchagua mtu ambaye hata mawasialiano ya Rais ambaye ndiye mwenye pesa hana atawasaidiaje kutatua changamoto zetu?”- Dr. Tulia Ackson

“Ndugu zangu tusidanganywe na watu ambao hawana hoja na kutuletea ahadi hewa hapa, wote tunafahamu Serikali yetu ni ya Chama Cha Mapinduzi, Mawaziri wote wanatokana na Chama Cha Mapinduzi sasa asitokee mtu akatuambia mara oooh! Atafanya hiki na kile wakati anajua hana huo uwezo hata wa kuwasiliana na Serikali ikamsaidia maana yeye hatujui hata chama chake kinaitwaje”-Dr. Tulia Ackson



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini