STAA wa filamu za kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amesema anamshukuru Mungu kwa kumsaidia kumlea vizuri mdogo wake Erick mpaka sasa amefanikiwa kuhitimu elimu yake ya msingi Shule ya Feza Boys.
Akizungumza na Mikito Nusunusu, mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake, alisema kuwa anatamani kuzungumza ni jinsi gani anavyojisikia vizuri kuona mtoto anayemlea tangu akiwa mdogo anazidi kuwa kijana bora machoni mwa watu.
“Namshukuru Mungu kwa hili, kulea sio kazi ndogo kuna muda naweza kusema Erick sio mdogo wangu bali ni mwanangu kwa sababu nimeanza kumlea tangu akiwa mdogo mpaka hapa alipofikia leo, ni jambo jema kuona ameshahitimu elimu yake ya msingi na muda si mrefu ataenda kujiunga na elimu ya sekondari, natamani kulia kwa hii hatua niliyofikia,” alisema Lulu anayefanya poa kunako anga la Bongo Muvi.
STORI: MEMORISE RICHARD
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments