Na Woinde Shizza, ARUSHA
Uongozi wa kijiji cha chemchem wilayani Karatu, wamehimizwa kuanza kutenga maeneo kwa ajili ya malisho ya mifugo, ili kusaidia ufugaji wenye tija na unaolenga kupata mifugo yenye afya bora.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Abbas Kayanda wakati akizindua maonesho ya tatu ya uogeshaji wa mifugo yenye kauli mbiu ‘kuogesha kwa afya na ufugaji wenye tija” uliofanyika kiwilaya katika kijiji cha Chemchem kata ya Rhotia, ambapo alisema lazima wafugaji waanze kutenga maeneo kwa ajili ya malisho ili kusaidia mifugo kupata chakula wakati wote, Na si kutenga tu bali kufuata maelekezo ya kitaalamu kujua ni aina gani za nyasi zinatakiwa kwa mifugo.
Kayanda alitoa wito kwa wafugaji kuacha ufugaji huria na badala yake kufanya ufugaji wa kisasa ili kuongeza ubora wa bidhaa zao ili tuweze kupata soko zuri na kuinua hali ya maisha yetu.
Alisema serikali kwa kulitambua hilo ndio maana imeanzisha uogeshaji wa mifugo , Kuogesha mifugo inasaidia kukinga mifugo na maradhi lakini pia inasaidia mfugo kuwa na afya bora ,Ambapo pia imeenda mbali ndio maana imetaka kuwe na kamati za usimamizi wa majosho.
Kayanda alisema kuogesha mifugo haimaanishi kuogesha ng’ombe peke yake tunatakiwa tuogeshe ng’ombe mbuzi kondoo na hata punda ,ukiogesha baadhi ya mifugo na kuacha mifugo mingine tatizo la magonjwa litaendelea kuwepo, Mifugo ambayo haijaogeshwa ni rahisi kuaambukiza mifugo iliyoogeshwa.
Wafugaji lazima wazingatie usafi wa zizi la ngombe, zizi linatakiwa kufanyiwa usafi na kupigwa dawa ili kuuwa mazalia ya kupe, alisema kama mifugo itaoshwa na kurudishwa kwenye zizi ambalo halikufanyiwa usafi na kupigwa dawa bado tatizo linakuwa halijatatuliwa.
Kayanda alielekeza Maafisa Mifugo kukaa karibu na wafugaji na kuwapa elimu juu ya ufugaji wa kisasa ,Lakini pia kutoa elimu ya namna wafugaji wanaweza kutenga sehemu ya maeneo yao ya kilimo kwa ajili ya malisho, kwa ajili ya ufugaji wa kisasa itawasaidia wafugaji kunufaika na mifugo yao na kuboresha hali ya maisha kuanzia kipato cha mtu mmoja mmoja na familia kwa ujumla.
Kayanda aliwaambia wafugaji wa kijiji cha Chemchem ikifika wakati wa kuchangia fedha kwa ajili kununua dawa za majosho wawe tayari kuchangia ,Kila mfugaji atakayechangia ahakikishe anapewa risiti,itaondoa changamoto za ubadhilifu wa fedha kwenye uendeshaji wa Majosho.
Awali Afisa mifugo wa wilaya ya Karatu Denis Buberwa alisema kuna lita 162 zilizogawiwa na serikali kwa ajili ya zoezi la kuogesha wa mifugo wilayani Karatu, Madawa ya kuogesha mifugo yanakuja kwa mwaka mara mbili na Wilaya ya karatu mpaka sasa ina jumla ya majosho 15.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments