Mahakama ya Ubelgiji yasema jino la shujaa wa DRC, Patrice Lumumba lirudishwe | ZamotoHabari.



Mahakama mjini Ubelgiji imeamuru kwamba jino lililochukuliwa kutoka kwa maiti ya shujaa wa Uhuru wa taifa la DRC wakati huo ikiitwa Congo Patrice Lumumba linapaswa kurejeshwa kwa familia yao, vyombo vya habari nchini Ubelgiji vimeripoti.

Lumumba aliyekuwa waziri mkuu wa Congo baada ya kujipatia Uhuru kutoka kwa Ubelgiji 1960, aliuawa 1961 baada ya kutekwa na wapiganaji waliotaka kujitenga.

Serikali ya Ubelgiji ilihusika katika kifo chake na mwaka 2002 iliomba msamaha rasmi.

Vitengo vya ujasusi vya Uingereza na Marekani pia vinadaiwa kuhusika.

Jino la Lumumbua linadaiwa kuchukuliwa na afisa wa polisi wa Ubelgiji aliyekuwa anasaidia kuuzika mwili wake , chombo cha habari cha AFP kimeripoti.

Baadaye jino hilo lilichukuliwa na mamlaka ya Ubelgiji , AFP kinaongezea.

Kwa mujibu wa BBC. Mahakama hiyo ya Ubelgiji ilisema kwamba jino hilo sasa linafaa kupewa mwana wa kike wa Lumumba Juliana Lumumba , ambaye aliandika barua kwa mfalme huyo wa Ubelgiji akiomba lirudishwe, mtandao wa Brussels Times uliripoti.

Kulingana na mtandao huo uamuzi huo wa mahakama siku ya Alhamisi unafuatia uamuzi mwengine wa ofisi ya kiongozoi wa mashtaka wa kijimbo kwamba mabaki ya Lumumba yanaweza kurudishwa kwa familia yake,



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini