Afisa Ununuzi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Frank Yesaya akitoa mafunzo kwa Wakurugenzi wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma pamoja na kanuni zake Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Timu ya Wataalam kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).
Mkurugenzi wa Ugavi na Ununuzi Bw. Arbogast Waryoba (kulia) akieleza jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyotolewa kwa Menejimenti kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya mwaka 2011 na mabadiliko yake ya mwaka 2016. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Felister Shuli.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara na Vitengo, Wakurugenzi Wasaidizi pamoja na Sekretarieti kutoka Kitengo cha Ugavi na Ununuzi wakisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa na Wataalam kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
OWM – KVAU
……………………………………………………………………………
Na; Mwandishi Wetu, OWM – KVAU
Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imepatiwa mafunzo na Wataalamu kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya mwaka 2011 na mabadiliko yake ya mwaka 2016 ili kuwajengea uwezo zaidi katika suala la ununuzi na kusimamia mikataba ya ununuzi wa umma pamoja na kuhakikisha mikataba inayoingia baina ya Ofisi na Wazabuni haileti kasoro yoyote.
Mafunzo hayo yamefanyika hii leo Oktoba 20, 2020 katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la PSSSF, Jijini Dodoma.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments