MKURUGENZI MKUU TANTRADE AKUTANA NA WADAU WA KLINIKI YA BIASHARA | ZamotoHabari.

 



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Edwin Rutageruka (Tan Trade) akiongoza kikao maalumu cha wadau wa Kliniki ya Biashara kutoka Taasisi za Umma na binafsi na kueleza kuwa lengo la kikao hicho ni  kufanya tathimini na kujadili mikakati ya maboresho ya utoaji wa huduma ya Kliniki ya Biashara.


Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Edwin Rutageruka amefungua kikao cha Wadau wa Kliniki ya Biashara kutoka Taasisi Binafsi na Taasisi za Umma zikiwemo EPZA, BRELA, TIC, GS1, TRA, WMA, NBC, NEEC, TBS, SIDO, FFC, CBE, na TFS. Lengo la kikao hicho ni kufanya tathimini na kujadili mikakati ya maboresho ya utoaji huduma ya Kliniki ya Biashara.

Kliniki ya Biashara husimamiwa na TanTrade na kudhaminiwa na Benki ya NBC ambapo huwakutanisha wataalamu wa Biashara kutoka Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi ambao hushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wafanyabiashara  nchi.

Itakumbukwa kuwa tarehe 14 Oktoba, 2020 Tanzania kupitia huduma ya Kliniki ya Biashara inayosimamiwa na TanTrade ilitajwa kuwa mshindi wa tatu wa dunia(Best use of partnership category) na wa pekee kutoka nchi za Afrika kwenye Tuzo za Taasisi zinazosimamia Biashara duniani (WTPO Awards 2020.)



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini