NYANDA ZA MALISHO LAZIMA ZIHIFADHIWE | ZamotoHabari.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Kimoukuwa wakiwa wanampokea mgombea ubunge katika jimbo la Longido Dkt.Stephen Kirushwa katika viwanja vya shule ya msingi Kimokuoa iliyopo katika Tarafa ya Longido

Mgombea ubunge jimbo la Longido Dkt.Stephen Kiruswa akiwa anafurahi mara baada ya kupokelewa na kundi kubwa la morani kulia kwake ni mwenyekiti wa CCM( w)ya Longido na baadhi ya viongozi wa kamati ya siasa 

Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Dkt.Stephine Kiruswa akizungumza na wananchi wa kata ya 
Kimokouwa 

Wazee jamii ya Kimaasai kutoka kata ya Kimoukouwa wakifuatilia kwa makini na kusikiliza sera za mgombea ubunge katika jimbo la Longido Dkt.Stephen Kiruswa

Wananchi 
 jamii ya Kimaasai kutoka kata ya Kimoukouwa wakifuatilia kwa makini na kusikiliza sera za mgombea ubunge katika jimbo la Longido Dkt.Stephen Kiruswa 

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Longido akisaini kitabu cha wageni katika kata ya 
Kimoukouwa alipokwenda kumnadi mgombea ubunge katika jimbo hilo.

======  == ====  ========
Na.Vero Ignatus,Longido

Sera ya Ardhi iliyopo inaruhusu kupimwa Nyanda zote za malisho, na kupatiwa hati miliki, pamoja na kuweka maji pale penye uhitaji wa ni muhimu kwa jamii ili ziweze kuendelea kuwepo kwa kizazi cha sasa na kile kijacho kwa manufaa ya jamii mzima ya wafugaji

Hayo yamesemwa na Dkt.Stephen  Kiruswa mgombea ubunge katika Jimbo la Logido kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi (CCM) katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji na Kata ya Kimokouwa Tarafa ya Longido mkoani Arusha kwamba ni lazima nyanda za malisho zihifadhiwe  

Kiruswa alisema Dkt.Magufuli ameruhusu wawekezaji kuwekeza katika sekta ya bidhaa za mifugo ,ambapo katika kata ya Kimokouwa kumejengwa kiwanda kikubwa cha kuchakata nyama na bidhaa za mifugo, jirani na mpaka wa Namanga kijiji cha Oryendeke,  ambapo kiwanda hicho kimekaribia kumalizika hivyo ni kwaajili ya watanzania wote ambapo mnufaikaji namba moja ni mfugaji wa Longido

Alisema katika kiwanda hicho zipo fursa kuu tatu kwa wakazi wa longido ikiwemo; kununua,kunenepesha na kuuza mifugo,ajira ambapo katika eneo hilo lilipojengwa kiwanda pana soko la kimataifa la mazao,pamoja na la kuuza na kununua mifugo hivyo wanawake watapata maeneo ya kuanzisha biashara za bidhaa za ngozi kwaajili ya watalii

''Tumeshamuomba mwekezaji shughuli zote ambazo wakazi wa eneo hilo wanaujuzi nazo wapewe wazifanye kwajili ya kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi , na kuondokana na kero ndogondogo za maishs ya kila siku.Alisema Kiruswa''

Alisema kuwa katika miaka hiyo mitano ijayo  wataendelea kuboresha sekta ya mifugo ,kwa kuhakikisha kwamba dawa za chanjo za mifugo, zinapatikana pamoja na kuhakikisha kuwa majosho yote yanafufuliwa, pamoja na kujenga mapya sambamba na kusimamia masuala ya masoko

Akizungumzia masuala ya barabara Kiruswa alisema kuwa barabara ni kama mishipa ya damu hivyo barabara hizo  ndizo zinazopeleka maendeleo vijijini na kwenye vitongoji kwamba yeye atasimamia sera hiyo pamoja na madiwani watakaochaguliwa katika uchaguzi siku chache zilizosalia

 Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya Joseph Sadira  aliwataka wanalongido kumuunga mkono Dkt. Sphen Kiruswa kwasababu amefanya shughuli nyingi za maendeleo  kwa muda mfupi alioingia Bungeni katika jimbo hilo

Sadira alisema katika sekta ya elimu  aliweza kushirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha kuwa wanaendeleza ujenzi katika shule zilizopo katika jimbo hilo na kuhakikisha shule zilizopo ambazo hazijasajiliwa zinasajiliwa kwa utaratibu uliowekwa na serikali.


 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini