Daftari la wapiga kura Uganda lapelekwa Uholanzi kuhakikiwa | ZamotoHabari.

 


Gazeti la Daily Monitor la Uganda linaripoti kuwa daftari la kitaifa la wapiga kura limepelekwa Uholanzi kwa ajili ya kuhakikiwa.



Tume ya uchaguzi imeipa zabuni kampuni ya Uholanzi kuondoa majina ya watu walioandikishwa zaidi ya mara moja wakati nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Januari.


“Tumeanza mchakato wa kuwathibitisha wapiga kura ili kuhakikisha kuwa wapiga kura wanaostahili tu wanaonekana kwenye daftari na kwamba watapiga kura mara moja,” msemaji wa tume hiyo Paul Bukenya amenukuliwa akisema.


Haijulikani kama vyama vya siasa vilijulishwa kuhusu hatua hiyo.


Raia wa Uganda watapiga kura kuchagua rais na wabunge tarehe 14 mwezi Januari. Wagombea 11- akiwemo Rais Yoweri Museveni- watawania nafasi hiyo ya juu.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini