Leo Novemba 27, 2020 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof. Ibrahim Hamis Juma, amewaapisha Mahakimu Wakazi 39 ambapo amewataka kuzingatia sheria na kuongozwa na taratibu,kanuni na nyaraka zinazotolewa mara kwa mara na viongozi wa Mahakama.
Akizungumza katika hafla hiyo Mheshimiwa Jaji amesema kazi ya Uhakimu sio kazi ya kuchukuliwa kimazoea au kwa wepesi wepesi bali uamuzi utagusa uhai,mali na hali ya wanadamu wengine na watanzania kwa ujumla.
''Mtatekeleza mamlaka ya utoaji haki kupitia mahakama zitakazokuwa huru na mtalazimika kuzingatia tu masharti ya katiba na yale ya sheria za nchi'' amesema Jaji Mkuu
Aidha amewakumbusha kuwa makosa yao yanaweza kusababisha wahalifu kama wa madawa ya kulevya wezi,wabakaji kurudi kwenye jamii na kuendeleza uhalifu huo na pia kuwapa moyo wahalifu wengine.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments