Marekani yashutumu vurugu zilizotokea Uganda baada ya kukamatwa kwa Bobi Wine | ZamotoHabari.

 


Marekani imeshutumu ghasia zilizojitokeza katika mji mkuu wa Kampala na miji mingine nchini Uganda kufuatia kukamatwa kwa mgombea wa urais Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine.

Ujumbe wa Marekani umesema kuwa "pande zote zipinge vita" na kuchukua hatua za kupunguza wasiwasi uliotanda nchini humo.


Bobi Wine alikamatwa wakati wa mkutano wa kampeni kwa madai ya kukiuka miongozo ya kukabiliana na virusi vya corona iliyowekwa na Tume ya uchanguzi.


Hata hivyo, muda mfupi baadaye wafuasi wake walianza maandamano wakidai aachiliwe huru.


Polisi wamesema watu watatu waliuawa huku wengine 34 wakijeruhiwa.


Uganda itafanya uchaguzi wa urais mnamo mwezi Januari 2021.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini