Ripoti ya utafiti wa rushwa ya ngono vyuoni wazinduliwa Dar | ZamotoHabari.

Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Denis Lekayo akisoma ripoti ya utafiti  uliofanywa kuhusiana na rushwa ya ngono katika vyuo vikuu vya Dodoma (UDOM) pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika mkutano wa uzinduzi ripoti hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Wildaf, Anna Kulaya akizungumza kuhusiana na harakati zinazofanywa katika mapambano ya rushwa ya ngono katika mkutano wadau uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake (WFT), Mary Lusimbi akitoa maelezo kuhusiana na utafiti wa rushwa ya ngono katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wakiwa na ujumbe wakionesha namna walivyoipokea ripoti ya rushwa ya ngono ya vyuo vikuu.
Wadau wa jeshi la polisi wakifatilia ripoti ya rushwa ya ngono iliyozinduliwa.
Baadhi ya wadau wakati uzinduzi wa ripoti ya rushwa ya ngono vyuo vikuu.

*Utafiti umebaini asilimia 50 ina uelewa wa rushwa ya ngono 

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Rushwa ya ngono imekuwa ikifanyika katika vyuo vikuu nchini kwa baadhi ya wahadhiri kwa kutumia mamlaka yao kufanya ushawishi wa ngono na baadhi ya wasichana kwa ajili kuwapa viwango visivyoendana na uwezo wao.

Baadhi ya wasichana ambao wamekuwa wamekuwa hawataki kutoa rushwa ya ngono wamekuwa wakipata wakati mugumu katika masomo yao.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru)  kwenye baadhi ya vyuo  umebaini kuwepo kwa rushwa ya ngono vyuoni hivyo wadau hawatakiwi kuupuza kwa kupigia kelele na wahusika wanaofanyiwa rushwa hiyo kuvunja ukimya kwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vinavyohusika ili kuchukua hatua kwa wahusika  kujenga jamii iliyo na maadili.

Hayo yamesemwa na Mwendesha mashitaka wa Takukuru Denis Lekayo wakati akisoma ripoti ya utafiti ikiwa ni maadhimisho ya Siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema utafiti huo umefanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na Mfuko wa Wanawake Tanzania  (WFT) katika vyuo vikuu viwili ambavyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) kwa  kipindi cha Januari na February mwaka 2019.

Lekayo amesema kufanyika katika vyuo hivyo  ni kutokana na historia ya vyuo hivi, umiliki wake (vyuo vya umma) na wingi wa udahili wa wanafunzi na  ni vyuo vikuu vikubwa  vinavyomilikiwa na serikali.

Lekayo amesema walihojiwa  katika utafiti huo ni Watu 589 Kati ya hao UDSM 352 na UDOM 237. Utafiti huu umetumia mbinu ya uchunguzi lengo la kupata taarifa za kina namna rushwa ya ngono kwa wasichana wa vyuo namna inavyotendeka. 

Amesema matokeo ya utafiti yanaonyesha wanafunzi waliohojiwa asilimia 81.6 na Watumishi 91.4 walikuwa na uelewa wa dhana ya rushwa ya ngono.

"Kuna mhadhiri mmoja kwa aibu alisema hatamani kuwa sehemu ya taasisi kutokana kuwepo kwa hali hiyo na kudai kuwa katika kupambana kunahitaji kuimarisha mifumo ndani katika vyuo"amesema Lekayo.

Amesema matokeo yanaonyesha zaidi ya asilimia 50 ya waliohojiwa walieleza uwepo wa rushwa ya ngono katika vyuo vikuu vilivyofanyiwa utafiti na kufanya suala hilo kunamaanisha kwamba rushwa ya ngono ni tatizo katika vyuo vikuu hivyo.

Hata hivyo amesema utafiti huo ulitaka kujua sababu zinazochochea rushwa ya ngono katika vyuo vikuu kwa kuwataja wahojiwa kueleza chanzo cha kuwepo vitendo vya rushwa ya ngono.

" Matokeo  ya utafiti vyuo vyote viwili  yanaonyesha kuwepo kwa sababu tano ambazo ni ukosefu wa maadili, ushawishi wa mtu mwenye mamlaka, mfumo wa utoaji taarifa kutokuwa rafiki, mifumo dhaifu ya kushughulisha rushwa ya ngono na mamlaka ya kutoa alama za mitihani kuachwa kwa wahadhiri  pekee." amesema Lekayo 

Lekayo amesema katika utafiti huo wamebaini matumizi mabaya madaraka ya kujinufaisha kingono kwa kutoa alama ambazo haziendani na mfanyiwa ngono.

Aidha, amesema kwa upande wa uadilifu mdogo, uongozi na kamati za maadili zinatajwa kutokuwa na maadili na wakati mwingine kamati ya maadili wao wenyewe wanafanya vitu ambavyo vinawafanya watu wasiwaamini na kuna mhadhiri ana ushawishi mkubwa katika kutenda vitendo vya rushwa ya ngono.. mara nyingi malalamiko yanayopelekwa na  hayashughulikiwi kutokana mhadhiri kuwa sehemu ya ngono hizo.

Ukosefu wa maadili kwa baadhi ya viongozi na wajumbe wa kamati za maadili kunasababisha kukosekana kwa uwajibikaji Jambo linalosababisha watumishi na wanafunzi kupoteza imani kwa uongozi wa kamati hizo.

Lekayo amesema wahadhiri wapya wanatambua kuwepo kwa muongozo na kanuni za maadili licha ya kudai kutoziona kutokana na upatikanaji wake kutokuwa rahisi.

"Hali hiyo inadhihirika wakati wa utafiti ambao ulikuwa vigumu kupata nyaraka hizi zinazosimamia sera, mifumo na muongozo. Wakati wa utafiti ilibainika nyaraka hizi hupatikana wakati mtumishi ama mhadhiri anapopata matatizo ya kimaadili," amedema Lekayo.

Amesema kitendo cha kuvuja  taarifa waathirika wa rushwa ya ngono  wengi wamekuwa waoga kutoa taarifa pale wanapobainika au wanapoombwa rushwa hiyo huku vitendo vya rushwa ya ngono vinakiuka kifungo cha 25 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 kinachokataza rushwa ya ngono.

Lekayo amesema mtumishi yeyote wa chuo Kikuu mwenye mamlaka ama madaraka anayetumia nafasi yake kumuwekea kigezo cha kupewa ngono mwanafunzi  au mtumishi mwenzake anayetaka huduma anakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa sheria hiyo.

Aidha, alisema utafiti ulilenga kubaini njia na mbinu zilizotumiwa kufanya ushawishi wa rushwa ya ngono katika tasisi za elimu ya juu.

Amesema matokeo yanaonyesha kuwa mbinu ya utoaji wa alama za chini kwenye mitihani iliongoza kwa kutajwa na wahojiwa ikifuatiwa na vitisho vya kutofaulu kwa wanafunzi.

Lekayo alisema wahadhiri hutumia mwanya huo kwa kuwapa alama ndogo  za masomo, kubadilisha alama za ufaulu, kuwafelisha au kuzuia matokeo yao ili kuandaa mazingira ya kuwashawishi kingono huku akidai kuwa kuna mwanafunzi wa Chuo Kikuu Muzumbe amefeli wanafuatilia huku mawasiliano hawayapati. 



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini