Dk. Mohamed Madkour
Imebainishwa kuwa urahisishwaji wa upatikanaji wa simu janja kwa bei rahisi ni miongoni mwa njia mahususi zaidi zinazoweza kuchochea uhamiaji kuelekea matumizi ya teknolojia za 4G na 5G katika bara la Afrika.
Ujumbe huo umebainishwa kupitia mkutano wa tano kuhusu mawasiliano ya internet barani Afrika wa Huawei uliofanyika kuanzia tarehe 9-12 Novemba
Katika mkutano huo ilibainishwa kwamba tasnia ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (ICT) bado haijaweza kuwa umuhimu zaidi kwa jamii, na kwamba kwasasa tasnia hiyo ipo mstari wa mbele katika kuleta maendeleo ya kijamii na kurejesha uchumi ulioathiriwa na janga la COVID-19.
"Muunganisho kupitia teknolojia ya mawasiliano ni msingi wa mabadiliko ya kuelekea ulimwengu wa kidigitali," alisema Dk Mohamed Madkour ambae ni Makamu wa Rais, Biashara Masoko na Ufumbuzi kutoka kampuni ya Huawei.
"Ni wakati sahihi sasa kushughulikia uunganisho wa mawasiliano ya internet sio tu kwa vigezo vya kasi , uwezo au ukubwa wa eneo, bali pia kwa ufikiaji wa mfumo mzima, bei nafuu, urahisi na thamani." aliongeza
Kwa mujibu wa ripoti ya GSM, idadi ya watumiaji wa mtandao wenye kasi ya 4G barani Afrika initarajiwa kuongezeka mara tatu katika miaka mitano ijayo, na huku idadi ya watu ikitarajiwa kuongezeka kutoka 55% leo hadi 80% mnamo 2025.
"Uunganishaji wa ulimwengu barani Afrika unahitaji ushirikiano thabiti kutoka kwa wadau wote ili kukuza biashara zenye faida na pia kuhimiza uwekezaji," alisema Madkour.
Roy Zheng, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Ng'ambo kutoka mmoja ya kampuni zinazotengeneza ‘semiconductor’, alisema kuwa tangu kuanza kwa janga la COVID 19, mahitaji ya vifaa hivyo vinavyotumika kutoa elimu yaliongezeka . Ili kukidhi mahitaji hayo, kampuni yake ilikuwa ikitoa ‘chipsets’ ambazo zinawezesha utengenezaji wa vifaa hivyo kwa bei iliyoanzia Dola za Kimarekani 48$.
"Kuhamia kwenye teknolojia yenye ufanisi zaidi na gharama ya chini kunaweza kuchochea uhamiaji kuelekea teknolojia ya 4G," alisema Zheng. "Tuna uwezo wa kutoa ‘chipsets’ hadi kwenye simu zenye bei inayoanzia dola $ 31 , ambayo inaweza kuwa simu muafaka kwa cha kiwango cha kuingia katika uhamiaji wa 4G." alisema.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Lin Ranhao, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya Tele 1 alisema kuwa katika miaka ijayo, ukuaji wa haraka zaidi wa wigo wa watumiaji wa 4G unatarajiwa kutoka barani Afrika.
Ranhao alisema Afrika ina watumiaji wengi wa 2G wanaosubiri kubadili kuelekea 4G, lakini licha ya miundombinu iliyo tayari, upenyaji wa 4G bado ulikuwa polepole. Akipendekeza njia za kutatua hili, Ranhao alitoa mlinganisho na China, ambayo ilikuwa inahimiza uzalishaji na ununuzi wa magari ya umeme kupitia ruzuku.
"Ikiwa uhamiaji kutoka 2G hadi 4G ni jukumu la dharura, tunapaswa kuchukua mkakati wa kufanya kazi zaidi, na kuendesha mchakato huu kupitia ruzuku. Kwa kweli kwenye hili la utoaji wa ruzuku ili kubeba mzigo wa watuamiaji ni jambo la kawaida ulimwenguni
Ranhao alisema mipango ya ruzuku pamoja na uuzaji wa simu janja kwa bei ndogo vitapunguza changamoto kwa wanunuzi wa kwanza wa simu janja, kuharakisha uhamiaji wa 4G na kufungua fursa kubwa kwa biashara, na kwa maendeleo ya binadamu.
"Kanuni ya mahitaji na usambazi ni nguzo muhimu ya biashara hii," alisema Madkour. "Miundombinu na wigo huwakilisha upande wa usambazaji, wakati huduma na mfumo wa ikolojia ni upande wa mahitaji. Tunaweza kukuza biashara ya watumiaji kwa kuonyesha dhamana ya ushirikiano katika mifumo ya mazingira na vifaa vya bei nafuu. ” aliongeza.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments