Ingawa tafiti kadhaa zilizopita ziliwahi kueleza kuwa ni vyema kunywa kiasi fulani cha pombe kwa afya yako, utafiti mpya umebaini kuwa pamoja na hayo, kuna hatari kubwa ya kuvuruga mwendo wa mapigo ya moyo kwa kunywa pombe.
Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na timu ya wataalam wa sayansi wakiongozwa na Profesa Peter Kistler wa Hospitali ya Alfred iliyoko Melbourne nchini Australia, pombe ina madhara mengi kwenye mwili wa binadamu ambayo yanaweza kuchangia katika kuvuruga mwendo wa mapigo ya moyo.
Imeeleza kuwa hali hiyo inaweza kuwa chanzo cha magonjwa ya moyo pamoja na stroke (kupooza).
Imeeleza kuwa kunywa pombe kunaweza kusababisha udhaifu katika moyo na inaweza kuharibu mfumo wa mawasiliano unaoweza kusaidia seli za misuli ya moyo pamoja na mfumo wa fahamu ambao unasimamia kazi nyingi za mwili.
Watafiti hao wamewashauri watu ambao hunywa pombe lakini wamekuwa wakisikia mwendo wa mapigo ya moyo hauko vizuri wasitishe ama kupunguza kwa kasi kubwa matumizi ya vilevi.
Wakizungumzia kiwango cha pombe ambacho kinamfaa mtu ambaye ameanza kusikia mapigo ya moyo hayako sawa, apunguze hadi chupa moja ya pombe yenye kilevi cha kawaida na ahakikishe anapata siku mbili kwa kila wiki kutotumia kabisa kilevi.
Kazi hiyo ya watafiti hao iliyochapishwa kwenye jarida la American College of College of ardiology, ilifanya marejeo ya tafiti zaidi ya 100 na iliwahusisha takribani watu 900,000.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments